Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda, akihutubia wakati akifunga Kongamano la 25 la Wajiolojia Barani Afrika lililofanyika tarehe 14-16 Jijini Dar es Salaam. Wakati akifunga Kongamano hilo, Waziri Pinda amewataka watafiti barani Afrika kufanya tafiti ambazo zina mahusiano ya moja kwa moja na jamii ili tafiti hizo zitumike katika kuwazesha wananchi kufaidika na rasilimali zilizopo barani Afrika.
Baadhi ya Wajilojia kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wanaohudhuria Kongamano la 25 la Wajiolojia Afrika wakifuatilia hotuba ya kufungamano hiyo iliyosomwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda (hayupo pichani).
Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajiolojia waliohudhuria kongamano hilo kutoka nchi mbalimbali Barani Afrika. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Sadik Meck Sadik na Rais wa Wajolojia Afrika Profesa Aberra Mogassie.
Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam
Wajiolojia barani Afrika wametakiwa kufanya tafiti zenye uhusiano wa moja kwa moja na jamii na kuzionesha tafiti hizo ili ziweze kutumiwa kama ufumbuzi wa matatizo mbalimbali yanayolikabili bara la hilo, jambo ambalo litaiwezesha Afrika kunufaika na rasilimali zilizopo na hivyo kuchangia katika ukuaji wa uchumi , maendeleo ya watu na mapato ya mataifa yao.
“Najua watafiti wanaweza kusema serikali zetu hazitumii tafiti zetu, lakini mkifanya tafiti zenye uhusiano wa moja kwa moja na jamii, mkazitoa kwa jamii tutazitumia msizifungie makabatini,” amesisitiza Pinda.
Hayo yamebainishwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda leo jijini Dar es Salaam wakati akifunga kongamano la 25 la Wajiolojia barani Afrika na kueleza kuwa, ili Afrika iweze kuendelea na kufaidika na rasilimali zake, inahitaji kuzalisha wataalamu wengi katika taaluma ya sayansi ikiwemo wajiolojia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...