Bodi ya korosho Nchini Imetangaza Kuanza rasmi kwa ununuzi na uuzaji
wa korosho katika msimu wa 2014/2015 utakaonza tarehe 20 mwezi huu ili
wakulima waweze kuitumia vema fursa ya kuvuna mapema korosho zao kabla
ya nchi nyingine kuanza kuvuna.
Mwenyekiti wa bodi ya korosho Tanzania Mhe Anna Abdallah (MB)ameyasema
hayo akiongea na waandishi wa habari na kubainisha kuwa ili kufikia
azima hiyo ya kutumia fusa ya uvunaji mapema ni vizuri wadau wote
wanaohusika na uuzaji na ununuzi wakamilishe maandalizi muhimu kabla
ya msimu kufunguliwa rasmi ili kuepuka ucheleweshaji wa ununuzi na
uuzaji wa korosho msimu huu.
Kufuatia kikao cha wadau wa tasnia ya zao la korosho katika mkutano
wao mkuu wa mwaka uliofanyika mjini Masasi tarehe 9-10 mwezi huu
wakulima walikubaliana kuwa bei dira(mwongozo)ya korosho ghafi
daraja la kwanza kuuzwa na kuanzia tshs shilingi 1000/= kwa kila
kilomoja.
Ambapo korosho daraja la pili zitauzwa na kununuliwa kwa
shilingi 800/= kwa kila kilo moja ambapo alifafanua kuwa kuwa bei
hizo ni za mwongozo tu kwani bei halisi itategemea nguvu ya soko
ambapo inaweza kubadilika kutokana na Ushindani wa wanunuzi kupitia
minada
Aidha mwenyekiti huyo aliwataka wafanya biashara kujiandaa kufanya
malipo ya leseni za biashara hiyo kufuatia miaka ya nyuma leseni za
biashara zilikuwa zinatolewa bila malipo.
Hata hivyo kwa mujibu wa
sheria ya fedha namba 5 ya mwaka 2011,kuanzia msimu huu leseni za
ununuzi wa zao hilo zitatolewa kwa malipo Ambapo wanunuzi wa ndani
watalipia ada ya shilingi 750,000/= na wanunuzi wa nje walipia ada ya
dola za kimarekani 500/= kwa msimu
Ununuzi wa zao hilo umekuwa ukiyumba katika baadhi ya misimu hasa
kuhusiana na suala la bei kiasi cha kusababisha malalamiko na migogoro
hata vurugu kutoka kwa wakulima dhidi ya serikali,vyama vya msingi na
Ushirika
Awali katika mkutano wa wadau wa korosho, BODI zote za mazao nchini
zimetakiwa kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wakulima ili
kuwajengea matumaini ya kuzalisha kwa wingi na kwa viwango
vinavyohijtajika kwenye masoko ya ndani na nje na kuliletea taifa
fedha za kigeni.
Rai hiyo ilitolewa wilayani Masasi mkoani Mtwara na waziri wa
kilimo,chakula na Injinia Christopher Chiza alipokuwa akifungua
mkutano mkuu wa wadau wa korosho Tanzania uliofanyika wilayani Masasi
katika ukumbi wa Emirates
Waziri Chiza Alisema kuwa bodi zote za mazao hapa nchini zinatakiwa
zitatuwe matatizo ambayo wakulima wanakumbana nayo na kuwasababishia
washindwe kufikia malengo yao waliyoyakusudia kunakotokana na
viongozi wa bodi kukwepa kutimiza majukumu yao wanayotakiwa
kuyatekeleza.
"Kwa sasa kumekuwa na mwaya mkubwa kati ya bodi, Halmashauri za wilaya
na miji,mifuko ya pembejeo na wakulima inayosababishia kutofanya
vizuri na kumuacha mkulima akiwa kisiwani bila ya kupata msaada
kupitia bodi hizo hivyo suala kubwa ambalo linapelekea kuwepo na
mwanya huyo kunatokana na kutowashirikisha wakulima kwenye maamuzi
mbalimbali ikiwemo kwenye kufanya mahesabu ya uendeshaji yanayohusu
manunuzi,gharama za matumizi na malipo ya majaliwa ambayo ni kiini cha
mafanikio kwa mkulima wa mazao.
"Wakulima wa Tanzania wako tayari kuzalisha bidhaa za mazao yao na Ili
mkulima apewe matumaini ya kuzalisha mazao kwa tija bodi lazima ziwe
mstari wa mbele katika utendaji wa majukumu yake kwa ufanisi na
uaminifu zaidi na kutii sheria ya ushirika na kanuni zake kwakufanya
hivi kutamsaidia mkulima,"alimalizia Waziri Chiza
Mwenyekiti wa bodi ya korosho Mhe Anna Abdallah akifungua kikao cha wadau wa korosho kilichofanyika wilayani Masasi mkoani Mtwara kulia ni waziri wa kilimo na ushirika Injinia Christopher Chiza na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe Joseph Simbakalia. Kikao hicho kinajadili maendeleo na changamoto za zao hilo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...