UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union "Wagosi Kaya" umekanusha vikali taarifa zilizizoenezwa kuwa mlinda mlando wa kikosi cha Vijana wenye umri chini ya miaka ishirikini U-20 Fikirini Suleimani “Mapara" kuwa amesajiliwa na Klabu ya African Sports “Wanakimanumanu”

Umesema taarifa hizo hazina ukweli wowote bali Fikirini bado ni mchezaji halali wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga na ni miongoni mwa wachezaji watakaoonekana kwenye kikosi hicho msimu ujao.

Taarifa iliyotolewa leo kwa nyombo vya Habari kupitia msemaji wa Klabu hiyo Oscar Assenga zimeelezwa kuwa fikirini bado ni mchezaji halali wa timu hiyo kwa kusajiliwa hivyo taarifa ya kuwa amejiunga na Africa Sports hazina ukweli wowote ule.

 Assenga amesema kuwa ili wadau wa soka waweze kuthibitisha kuwa mchezaji huyo bado yupo kwenye kikosi cha wagosi hao wa kaya wafike mazoezini Jumatatu kwani atakuwepo.

Amesema kuwa Fikirini ni miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo msimu ujao wa Ligi kuu soka Tanzania bara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ivi ule upinzani ulikuwepo enzi hizo kati ya timu hizi mbili bado upo kweli???

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...