FAINALI za mashindano ya Ngoma za Asili ngazi ya mikoa zijulikanazo
kama “Balimi Ngoma Festival 2014” Mkoani Mwanza kikundi cha
Mwanalyaku cha chenye makazi Magu kimefanikiwa kuwaa ubingwa
wa Mkoa wa Mwanza na kuzawadiwa fedha taslimu Shingi 600,00/=
pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa wa Kagera katika fainali za Kanda
zinazotarajiwa kufanyika Augusti 16,2014 Mkoani Mwanza.
Nafasi ya pili ya mashindano hayo ilichukuliwa na Kikundi cha Bujora
cha Magu pia ambacho kilizawadiwa fedha taslimu Shilingi 500,000/=
pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa katika fainali za Kanda.
Nafasi ya tatu ilichukuliwa na kikundi cha Utandawazi cha Ukerewe
ambacho kilizawadiwa fedha taslimu Shilingi 400,000/= na nafasi ya
nne ilichukuliwa na kikundi cha Wadonho cha Sengerema ambacho
kilizawadiwa fedha taslimu shilingi 300,000/=.
Nafasi ya tano ilichukuliwa na kikundi cha Mwanza Sanaa na nafasi
ya sita ilikwenda kwa kikundi cha Ngoma Buhongwa ambavyo
vilizawadiowa fedha taslimu Shilingi 150,000/= kila kikundi. Jumla ya
Vikundi 6, vilijitokeza kushiriki fainali hizo za Mkoa wa Mwanza ngazi ya
Mkoa kwa Mwaka 2014.
Akizungumza na kwa nyakati tofauti Meneja matukio wa Kanda ya Ziwa,
Erick Mwayela alisema Sababu msinigi ya kuwepo kwa Mashindano ya
Balimi Ngoma za Asili ni kuenzi na kulinda utamaduni wa Kitanzania.
Mwayela aliongeza pia kuwa wao Kampuni ya Bia nchini ni sehemu yao
ya kurudisha fadhila kwa watumiaji wa Kinywaji cha Balimi Extra Lager
pamoja na vinywaji vyote vya Kampuni ya Bia Tanzania(TBL).
Fainali za Mkoa wa Mwanza zilifanyika katika Uwanja wa Polisi Mabatini
na fainali za Kanda za mashindano ya Balimi Ngoma zinatarajiwa
kufanyika August 16,2014 jijini Mwanza kwa kushilikisha vikundi viwili
viwili kutoka Tabora, Shinyanga, Bukoba, Musoma na Wenyeji wa
mashindano Mwanza.
Mabingwa wa fainali za mashindano ya Ngoma za asili yajulikanayo kwa “Balimi Ngoma Festival 2014”ngazi ya Mkoa, mkoa wa Mwanza, kikundi cha Mwanalyaku cha Magu wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutangazwa yaliyofanyika katika Uwanja wa Polisi Mabatini jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wakadhi wa jijini Mwannza wakishuhudia fainali za mashindano ya Ngoma za asili yajulikanayo kwa “Balimi Ngoma Festival 2014”ngazi ya Mkoa, mkoa wa Mwanza yaliyofanyika katika Uwanja wa Polisi Mabatini jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
Malenga wa Kikundi cha Mwanalyaku cha Magu jijini Mwanza akiimba wakati wa fainali za mashindano ya Ngoma za asili yajulikanayo kwa “Balimi Ngoma Festival 2014”ngazi ya Mkoa, mkoa wa Mwanza yaliyofanyika katika Uwanja wa Polisi Mabatini jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.Kikundi hicho kilitwaa ubingwa wa Mkoa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...