Ofisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Ambrose Manyanda akitoa huduma
ya elimu inayohusu Mfuko kwa mdau aliyetembelea banda la Mfuko kwenye maonesho ya
Nane Nane Mkoa wa Lindi.
Meneja wa NHIF Mkoa wa Lindi Fortunata Raymond akiwakaribisha akina mama kwenye
moja ya mabanda ya Mfuko kwa ajili ya kupata huduma ya upimaji wa Saratani huduma
inayotolewa na Mfuko kwenye maonesho hayo.
Wananchi wakisubiri kupata huduma ya upimaji afya bure katika banda la NHIF ambalo
huduma za upimaji zinatolewa bure.
Burudani ya ngoma na maigizo ikiendelea katika banda kla NHIF kwa lengo la kuelimisha.
Sehemu ya ushauri wa namna ya kujikinga na maradhi yasiyoambukiza ikiendelea na huduma
zake.
Huduma zikiendelea bandani hapo.
Kaya ya Said Mnyou ikiwa katika picha ya pamoja baada ya kujiunga na Mfuko wa Afya ya
Jamii (CHF), wananchi wanajiunga moja kwa moja kwenye maonesho hayo.
Kikundi cha sanaa kikiendelea na uhamasishaji wa wananchi kujiunga na CHF na kunufaika na
huduma zinazotolewa kwenye maonesho hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...