.jpg)
Mwanamuziki Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja mtunzi,mwimbaji kiongozi wa bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma africa band aka FFU Ughaibuni yenye makao yake nchini Ujerumani, amefunguka na machache yafuatayo kuhusu mabadiliko ya katiba mpya ya Tanzania na haki za raia wa Tanzania:
Akizungumza kutoka katika makao yake mjini Oldenburg,Ujerumani.
Kamanda Ras Makunja wa kikosi kazi FFU-Ughaibuni alisema
Kuwa: MCHAKATO WA KATIBA MPYA UMEWAFANYA WATANZANIA
WENGI KUSOMA KATIBA YA ZAMANI ! MWANZO WALIKUWA HAWAISOMI NA KULIELWA VEMA !
Kwa sasa ! WATANZANIA HATUNA HAJA YA KUOGOPA MAUMIVU YA
MABADILIKO YA KATIBA LAZIMA TUENDE KUFUATANA NA WAKATI,
LAZIMA TUWEKE MASALAHI YA TANZANIA NA MTANZANIA KWANZA,
Ras Makunja,alichambua zaidi kwa kusema kuwa watanzania tumekuwa tunatabia za uwoga wa maumivu ya mabadiliko linapokuja swala la kujadili masilahi ya kitaifa na mtanzania,mara nyingine bila ya kujijua tunawapigania
watu ambao sio walengwa katika katiba "Nina maana walengwa wa kunufahika katika katiba hii lazima wawe watanzania wote wa bara na visiwani ambao wanaishi popote pale duniani" bila kujali dini,jinsia au
vyama vyao vya kisiasa.
SWALI: NINI MTAZAMO WAKO NA UNATARAJIA NINI ? KATIKA KATIBA MPYA ?
RAS.MAKUNJA: Mtazamo wa wangu katika kulijadili hili la katiba mpya ningewaomba kwanza wale wabunge walio katika bunge maalumu la katiba
kwamba : WAFANYE KILA HALI KATIKA MJADALA HUU KUPATA KATIBA
YENYE MASILAHI 99% TANZANIA NA MTANZANIA KWANZA
Mfano: Haki za kumiliki Ardhi,tunapoongelea swala la Haki ya mtanzania
basi Ardhi na maslahi yanayo patikana katika Ardhi lazima yamilikiwe na
raia wa Tanzania kwanza,kwa sababu Ardhi ndio msingi au ubongo wa nchi yetu,kwa maana hii asilimia kubwa ya ardhi kama haipo katika miliki ya raia wa Tanzania ,uhuru wetu unatakuwa umepungua maana.
ARDHI NA RAIA WA TANZANIA NDIO MOYO WA TAIFA NA UTAWALA
WA TANZANIA,asilimia 50% ya Adhi ikiwa mikononi mwa watu ambao sio
watanzania,au watu ambao wana offer za kukaa au kufanya jambo katika
ardhi kwa mktaba wa miaka mingi ,wananchi tutajikuta tupo ugenini katika ardhi yetu.HII HAINA MAANA KUWA TUNAWAFUNGIA MILANGO WAWEKEZAJI BALI TUNAWEZA KUINGIA NAO MIKATABA YA MUDA MFUPI .
SWALI: KUHUSU URAIA PACHA UNALIONAJE HILI?
RAS MAKUNJA: SIO SWALA LA WENGI WAPE, NA WACHACHE WANYIMWE BALI SWALA LA HAKI YA BINADAMU NA URAIA
WATANZANIA LAZIMA TULITAZAME SWALA URAIA PACHA KWA FAIDA YA TANZANIA NA PIA TULICHAMBUE HASARA NA FAIDA ZAKE.
Ras Makunja aliingia kwa kina kwa kusema kuwa kuhusu uraia pacha
walio wengi wanahitaji kuelemishwa faida na hasara zake,pamoja na haki
za msingi kwa watanzania wanaomba hili liwemo katika katiba mpya.
Kwanza tunapolizungumzia hili lazima tujue nini ? maana uraia na nini maana Pasipoti. Historia inaonyesha kuwa matumizi ya PASIPOTI yalianza mapema mwaka 1910 SOVIET UNION (URUSI) ndio walioanzisha kwa nia ya kuwathibiti raia wao katika mfumo wa kikomunisti,baada ya hapo ndipo madola mengine yakafuata; Leo tunapoongelea uraia pacha wengine wanachanganya pasipoti tu za kusafiria na kusahau haki za uraia na binadamu kwa ujumla. Katika kanuni za haki za binadamu hairuhusiwi mtu kunyang'anywa uraia wake, Mimi ningeshauri kuwa katiba mpya iruhusu raia watanzania waweze kuwa na pasipoti zaidi ya tatu,kwa sababu zitawasaidia katika maswala la maendeleo,kama vile uchumi,elimu n.k
MFANO HAI KUNA WATOTO WALIOZALIWA NJE YA NCHI WAZAZI WAO WOTE NI WATANZANIA LAKINI WANAKOSA HAKI KATIKA NCHI WALIOZALIWA KWA KUWA SI RAIA WA NCHI ILE,NA WANAPOTIMIZA MIAKA 18 WANASHINDWA KUUKANA URAIA WA TANZANIA NA KUOMBA WA NCHI WALIOZALIWA JAPO NCHI WANAYOISHI WANAWEZA KUWA RAIA PACHA.
Watoto hawa wanasulubiwa kwa kuhukumiwa makosa ambayo hawajafanya ! kwani awakuomba wazaliwe ughaibuni, Watanzania katika katiba mpya lazima tuwafikirie watoto hawa wasio na hatia.
Hata katika kanuni za haki za binadamu zinasema kuwa "Si ruhusa kwa binadamu yeyote yule kunyanga'nywa uraia wake.Sasa mtoto wa kitanzania akiwa hana haki ya kuwa mtanzania kwa kuwa kazaliwa nje ya nchi ! hii si haki.
(B) Muwekezaji wa Kigeni anapokaribishwa Tanzania kwa maneno ya "Jisikie upo Nyumbani ! na mtanzania hakubaliki kwao hapa kidogo pana utata lazima patazamwe upya.
Kwa sasa kuna nchi nyingi duniani ambazo katika katiba zake zinasema kuwa raia wa nchi hizo harusiwi kuny'angwa uraia wake ata kama anaomba uraia wa nchi nyingine,sisi bado tunaogopa kulijadili kwa visingizio vya usalama. Kwa Sasa hatuna adui kama ilivyokuwa zamani tuliofu makaburu n.k Adui wetu wa sasa ni NJAA NA UMASIKINI na Uraia pacha unaweza kuwa silaha kubwa ya kupiga vita adui zetu hawa NJAA,UMASIKINI.
TUNAWEZA KUWEKA MASHARTI KWA WALE WATAKAO KUWA NA URAIA PACHA(Ras Makunja alisisitiza) Mfano: Mtu akiwa na uraia pacha hawezi kugombea nafasi za juu ya uongozi wa taifa kama vile mbunge,diwani, Rais. Au kufanya kazi katika sekta ya usalama na mambo nyeti yanayo husu taifa. huu ni mfano tu. Uraia pacha si swala la kuliogopa bali kuelimishana.
SWALI : MATEGEMEO YAKO KUHUSU KATIBA MPYA?
Ras Makunja: Ni mategemeo yangu kuwa wabunge katika bunge maalumu la katiba wataweka maslahi ya Tanzania na watanzania kwanza na kuondoa itikadi zao za ki-vyama kama tunanyoona sasa. Tunategemea watatuletea rasimu ya mapendekezo ya katiba yenye masilahi ya Taifa na watanzania kwanza si vinginevyo. mwanamuziki huyo alimalizia.
Kamnada mkuu,hongera sana kaazi yako ,kumbe pamoja na ukamanda wako kichwani mwako umejaa mengi yenye manufaa kwa nchi na raia wake
ReplyDeleteAfande kamanda ras makunja tulijua tu mindhari amiri jeshi mkuu JK kakupa amri wapi? pa kushamabulia basi umeanza na hoja ya haja,
ReplyDeleteMkuu wa kikosi kazi ughaibuni hoja yako ni ya msingi,lazima tuwafikilie watoto wa kitanzania walizaliwa nje tusiwahukumu kwa makosa ya kuazaliwa nje
ReplyDeletePasua ! Pasua ! Kamanda mkuu
ReplyDeleteKweli mkuu mchina hapa TZ anaona anajiona nyumbani wabongo wanafanyiwa roho mbaya
ReplyDeletehili swala ni dogo sana
ReplyDeletemtoto aliyezaliwa na wazazi watanzania ni mtanzania period
uraia pacha ruksa kwa mtu aliyeupata uraia wa pili by default kama hao watoto ... ILA ... raia yeyote wa tanzania kwa uamuzi wake mwenyewe akiamua kuomba uraia wa nchi nyingine atakua ameukana utanzania wake na uraia wake wa tanzania. Vivyo hivyo raia yeyote wa nje hataruhusiwa kupata uraia wa tanzania mpaka aukane uraia wake wa kwanza na kutukabidhi kithibitisho ambacho ni passport yake ya kwanza kwa processing na nchi husika.
mwisho mtu yeyote wenye uraia pacha hataruhusiwa kuwa na fursa ya kuwa kiongozi wa serikali, bunge wala mahakama hata kama ni udiwani!
watanzania bado tupo kwenye usingizi mzito kuhusu uraia pacha
ReplyDeletekamanda ras makunja's asante sana kwa hoja yako hii,unajua kuna watu bado wanachanganya mambo kuhusu uraia pacha,jambo hili halikwepeki kwa sababu kuna raia wa kigeni wanaomba uraia wa Tanzania,katiba ya nchi zao haziruhusu raia wao kuukana uraia wake wa asili kwa maana hii basi wanaruhusiwa kuchukua uraia wa nchi yeyote hila bila ya kurudisha uraia asilia,na kwa Tanzania hapo ndipo tuna wakubali raia hao wa kigeni na uraia wao pacha bila sisi kujitambua.
ReplyDelete