Narudi katika safu hii kwa ngoma ya "Kuch Kuch Hota Hai"
Na Sultani Kipingo
Kuch Kuch Hota Hai (tafsiri yake “kuna vitu hutokea”), ambayo pia
ilijulikana kama KKHH, ni filamu ya kuchekesha ya Kihindi iliyotoka India na
Uingereza Oktoba 16, 1998. Mwandishi na mwongozaji wake alikuwa Karan Johar na
wachezaji wake walikuwa Shahrukh Khan na Kajol, ikiwa ni filamu yao ya nne
pamoja. Ilipigwa India, Mauritius na Scotland, ikiwa ni mara ya kwanza kwa
Karan Johar kuongoza filamu, akiwa na lengo la kupiga hatua mpya katika filamu
za Kihindi.
Hadithi
yake inahusisha pembe tatu za aina mbili za mapenzi. Nusu ya kwanza inahusu
marafiki wakiwa chuoni, wakati nusu ingine inaelezea hadithi ya binti wa mjane
anayejaribu kuwaunganisha baba yake na rafiki wa zamani.
Filamu hii ilifanikiwa sana
India na ulimwenguni kote, ikawa ndiyo filamu iliyoingiza mapato makubwa kwa
mwaka huo wa 1998, na pia filamu ya kwanza ya kihindi kuingia katika filamu 10
bora za Uingereza. Wakati muziki wake nao uliuza sana kwa mwaka huo, filamu hii
ilijishindia tuzo kibao. Na hadi leo, pamoja kuwa ni ya siku nyingi, bado
inatazamwa katika TV za India.
Tunaipataje hiyo? jamani enzi za majumba ya cenema zilikuwa juu pia .... umetukumbusha delight cinema ya shinyanga enzi zile tuko shycom
ReplyDelete