Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), imedhamini kambi ya siku tano ya kuogelea iliyoandaliwa na Champions Rise Swimming Club. Kambi hiyo inayofanyika katika bwawa la kuogelea la shule ya Sekondari ya Shabaan Robert inaendeshwa na Kocha kutoka marekani pamoja na muogoleaji mwenye medali ya dhahabu, Penny Haynes.
Kambi hii inafanyika kwa mara ya kwanza kukiwa na muogeleaji bingwa wa dunia, Lengo likiwa ni kuwahamasisha waogeleaji wa Tanzania kufikia kiwango cha Kimataifa.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya sh. milioni 5 Ofisa Mwandamizi wa Uhusiano wa NSSF, Juma Kintu alisema, mchezo wa kuogelea ukipewa kipaumbele na serikali unaweza kuliletea taifa medali katika mashindano mbalimbali Duniani.
Mkufunzi wa kambi ya kuogelea ya watoto kutoka Marekani, Penny Haynes akisimamia mazoezi ya kuogelea.
Mkufunzi wa kambi ya kuogelea ya watoto kutoka Marekani, Penny Haynes akisimamia mazoezi ya kuogelea.
Ofisa Mwandamizi wa Uhusiano wa NSSF, Juma Kintu kakimkabidhi mfano wa hundi ya sh. milioni 5, Gidibo Tindwa kwa ajili ya kambi ya kuogelea ya watoto inayofanyika katika Shule ya Sekondari Shaban Robert jijini Dar es Salaam.

Picha ya pamoja.
Mwanafunzi wa Shule ya Bracburn iliyopo Arusha, Cornelia Bulengo akipokea zawadi kutoka kwa Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Juma Kintu.
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Aga Khan Mzizima, Shivani Bhatt akipokea zawadi kutoka kwa Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Juma Kintu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...