Chama Cha Mapinduzi kimewastukia Ukawa na kusema wanachofanya ni Usanii usiokuwa na tija mbele ya mambo ya msingi kwa Taifa la Tanzania, akizungumza na mwaandishi wa habari hizi Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye alisema hoja zote zinazotolewa na UKAWA zina majibu kwenye Sheria na Kanuni zinazoendesha Bunge la Katiba ,CCM pia imewashukia  UKAWA kwa kuwatukana na kuwadhalilisha viongozi wa dini ambao wamekuwa wakisisitiza UKAWA kurudi Bungeni.


     CCM yawaomba wabunge wa bunge la Katiba wanaotaka Katiba mpya waendelee na bunge  litakapoitishwa tarehe 5/8/2014.


Kwa taarifa za ndani ya kikao hicho ,kikao kimeisha kwa kukubalina kutokubaliana ,pande mbili hizi zimekutana zaidi ya mara nne pamoja na kikao cha leo kilichoanza tangia asubuhi saa nne mpaka jioni lakini hakuna hata pande mmoja uliokubalina na mwenzake.


Kwa mujibu wa taarifa za ndani Msajili wa vyama vya Siasa  nchi anatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari kesho jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. TAFADHALI SANA MHESHIMIWA NAPE USANII NDIO ULIOTUFIKISHA HAPA TULIPO SI RAHISI KWAKO KUKIRI MAKOSA MLIYOYAFANYA WAKATI WA MIKUTANO YA MABARAZA YA KATIBA NA VIKAO VYA AWALI VYOTE VYA KATIBA MPYA.
    MLICHOKITEGEMEA NI KUTULETEA KATIBA MPYA YA CCM SASA UKAWA NDIO KIKWAZO KWENU KWA SASA,PIA KATIBA MPYA SIO MALI YA CCM WALA MALI YA UKAWA NI MALI YA WANANCHI WOTE SASA HUONI KUWA WANACHOKIFANYA UKAWA NI KUHAKIKISHA KUWA WANANCHI NA RASIMU YA JAJI WARIOBA NDIO WASIKILIZWE SIO SERA WALA KATIBA INYOHITAJIKA NA CHAMA CHA SIASA CHOCHOTE.
    WAZO LANGU MUHIMU NI HILI KWA NINI HAMLETI RASIMU YA MWISHO YA JAJI WARIOBA KWETU WANANCHI TUAMUE TUNATAKA IWE HIVYO AU HATUTAKI?BADALA YA CCM KULAZIMISHA KUTAKA KUFANYA MAREKEBISHO YA SEREKALI MBILI HILO NDIO TATIZO KWA SASA NA LITAENDELEA KUWA TATIZO BAADAE IKIWA MTALAZIMISHA HILO.
    MIMI SIO MWANACHAMA WA CHAMA WA CHAMA CHOCHOTE CHA SIASA HAPA NCHINI KWA SABABU SIKUONA UMUHIMU WA KUFANYA HIVYO NA NI UHURU NA UAMUZI PAMOJA NA HAKI YA KILA RAIA WA NCHI HII SIO VITU VYA LAZIMA NDIO MAANA NINAONGEA HIVI UKAWA NI TATIZO KWENU NA KAZI YA UKAWA KWA SASA NI KUKUZUIENI NYIE CCM MSIBAMBIKE KATIBA INAYOTAKA IWE MAONI YA WANACHAMA WENU WOTE,BAADHI AU VIKUNDI TU VYA CCM WAO UKAWA NAO WANALOLITAKA WAMESHASEMA WAZI NI KUUNGA MKONO SEREKALI TATU NA KUPIGANIA RASIMU HALALI ILYOKO KWENYE MEZA SASA MUAMUZI NI MWANANCHI SIO VYAMA LETENI KWETU TUTAWAPATIA JAWABU MSITUJIBIE KAMA HATUNA MIDOMO.
    NAFIKIRI TUMEELEWANA HIKI SIO KIINGEREZA NI KISWAHILI KITUPU ACHENI USANII WA KITOTO TANZANIA HIVI SASA INA WENDA WAZIMU WACHACHE SANA WENGI WETU NI WENYE SIHA KAMILI NA AFYA KICHWANI HATUDANGANYIKI TENA WAHESHIMIWA.
    MDAU.
    UPANGA,DSM TZ.

    ReplyDelete
  2. Anayeweza kuyaweka sawa haya ni mtu mmoja rais jakaya mrisho kikwete hamna mwengine maana tunaye rais ana busara na hekma na kipaji cha kusuluhisha

    ReplyDelete
  3. Jamani kunapopiganiwa mambo mawili ya serikali tatu na mbili kuna kuwa na upinzani wa kushinda au kushindwa. Hata mechi ya mpira ni hivyo. Wao UKAWA waende bungeni wakacheze mpira wa serikali 3 na 2 na tuone mshindi ni nani kwa sababu wakisha jadili watarudi kwa wananchi watakachokisema wananchi ndicho hicho. Wakikaa uchochoroni ndio suluhu linapatikana huko. Ni sawa na kuinua mikono kwamba wameshindwa kufanya utetezi bungeni. Nendeni bungeni mwaogopa CCM?

    ReplyDelete
  4. huu siyo muda wa kutuhumu tena kwa maneno makali kama aliyotumia Nape Nnauye. pia hii lugha aliyotumia Nape wengine hatujaizoea kusikia ikitolewa na kiongozi wa chama cha mapinduzi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...