Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amekubali kumuondolea sakramenti ya upadri, Padri Raymond Mosha wa Jimbo la Katoliki la Moshi ikiwa ni miaka 20 tangu padri huyo aombe kujiondoa kwenye daraja hilo.
Barua ya uamuzi wa Papa Francis ilisomwa jumapili ya juzi katika parokia na vigango vyote vya Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi wakati wa ibada za jumapili zilifanyika katika makanisa ya jimbo hilo.
Miongoni mwa parokia ambazo barua hiyo ilisomwa ni Parokia ya Karanga ambako Paroko wake, John Matumaini alitoa tangazo hilo katika ibada zote. Uamuzi huo ambao ni nadra sana kutolewa na Papa, unamaanisha kuwa sasa hivi padri huyo yuko huru kuoa na kuwa na familia kama Wakristo wengine.
Hata hivyo, wakati uamuzi huo ukitangazwa rasmi juzi, tayari Padri Mosha ambaye ni profesa wa falsafa na maadili katika Chuo Kikuu cha Nelson Mandela Arusha, ana mke na watoto watatu ambao kwa sasa wako vyuo vikuu.
Padri Mosha alisema aliandika barua kuomba kuondolewa daraja hilo mwaka 1994 kabla ya uamuzi kutolewa juzi.
Katika orodha ya mapadre 185 wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi iliyopo katika tovuti ya jimbo hilo, jina la Padri Mosha linaonekana likiwa ni namba 23.
Akizungumzia hatua hiyo, Padri Mosha alisema: “Ninafurahi kufunguliwa kifugo hiki na hii itanifanya niishi kama Mkristo. Kwa vile hawajaniondolea sifa ya kutoa huduma kama vile ibada za mazishi, sakramenti ya mwisho na ubatizo, nitaendelea kutoa kwa wahitaji kwa sababu ninaupenda ukristo.
“Nashukuru sasa nimekuwa muumini wa kawaida nitaweza kufunga ndoa kanisani kwa kuwa nilikuwa nimefunga ndoa ya kisheria tu kwa DC.”
Kuhusu kwa nini aliamua kuacha upadri, Profesa Mosha alisema ni baada ya kufanya kazi hiyo kwa miaka 20 na akaona ipo haja ya kuwa na familia lakini kanisa lilikuwa haliruhusu.
“Sasa kwa kuwa kanisa haliruhusu mapadri kuoa ndiyo maana nikaamua kuandika barua ambayo hata hivyo, imechukua muda mrefu kujibiwa na tayari nina watoto watatu wako chuo kikuu.
HUREE HUREEE!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteTHIS IS GOOD NEWS.
THANKS PAPA, PLEASE ALLOW ALL PRIESTS AND SISTERS TO GET MARRIAGE.
MIMI NI MKATOLIKI NINASUPPORT MAPADRE NA MASISTER WAOE NA KUOLEWA.
MIAKA MIWILI ILIYOPITA NILIBAHATIKA KWENDA VATICAN ROME NA KUSHEHEREKEA MASS NDANI YA KANISA LA ST PETERS BASILICA WITH MY CHILDREN. LAKINI SIKUMUONA PAPA. WAZO AMBOLO NILIKUA NALO TOKEA NAFANYA MAFUNDISHO KATIKA KANISA LA ST THERESIA BARABARA YA 20 TANGA, ENZI YA SISTER MARTINA MIAKA YA 80.
KAMA KUNA MTU ANAJUA JINSI YA KUFANYA KUMUONA PAPA NAOMBA ANIELEZE NATAKA KWENDA TENA NIKAABUDU NA AWABARIKI WATOTO WANGU. I WILL GO AGAIN TOMORROW
THANKS
EDY UK
Safi kabisa umekuwa mkweli wengine wanaishi kinafiki kwa kujivinjari na watoto na wake za watu ndoa kibaao matatani kisa padri wanafiki kama kipindi cha 2004-2008 huku kijichi
ReplyDeleteSio mbaya lakini yafaa kamaka kanisa tuandae vizuri vijana ambao wataend mbele za bwana daima bila kugeukia malimwengu
ReplyDelete