Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa kushirikiana na Taasisi ya Flaviana Matata imetoa msaada wa vifaa vya shule kwa wanafunzi walio katika mazingira magumu mkoani Lindi.
Flaviana Matata ambaye ni mwanamitindo anayefanya nchini Marekani amekabidhi mabegi 650, kila begi lina vifaa mbalimbali vya shule.
Vifaa vilikabidhiwa na Flaviana Matata mwenyewe kwa baadhi ya wanafunzi wa wilaya za Nachingwea na Lindi Mjini
Lengo la msaada huo ambao umetolewa kwa pamoja kati ya Taasisi ya Flaviana Matata na PSPF ni kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha kila mwanafunzi nchini Tanzania anapata elimu akiwa na vifaa muhimu vinavyohitajika.
Hii ni mara ya pili kwa PSPF kwa kushirikiana na Taasisi ya Flaviana Matata kutoa msaada huo kwa wanafunzi, mwaka jana wanafunzi wa shule mbalimbali mkoani Pwani walifaidika na msaada huo.
Mfuko wa Pensheni wa PSPF umekuwa ukijihusisha katika kusaidia maeneo mbalimbali yanayohitaji msaada ambao utaleta mabadiliko chanya kwa jamii ya Tanzania.
Mwanamitindo Flaviana
Matata (wa tatu kutoka kulia waliosimama nyuma) akiwa katika picha ya pamoja na
baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi
Mnengulo mkoani Lindi. Jumla ya wanafunzi 650 wa shule zilizipo katika Halmashauri za Lindi na Nachingwea mkoa wa Lindi wamenufaika na msaada huo wa
mabegi hayo yenye vifaa mbalimbali vya shule, msaada huo umetolewa kwa pamoja
kati ya PSPF na Taasisi ya Flaviana Matata. Kushoto ni Meneja Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa Mfuko
wa Pensheni wa PSPF, Costantina Martin.
Afisa Uhusiano wa
Mfuko wa Pensheni wa PSPF Colleta Mnyamani akimpongeza mmoja wa shule ya Msingi
Mnengulo mkoani Lindi. Jumla ya wanafunzi 650
wa shule zilizipo katika
Halmashauri za Lindi na Nachingwea
mkoa wa Lindi wamenufaika na msaada huo wa mabegi hayo yenye vifaa
mbalimbali vya shule, msaada huo umetolewa kwa pamoja kati ya PSPF na Taasisi
ya Flaviana Matata. Nyumba ni Mwanamitindo Flaviana Matata.
Meneja Mawasiliano,
Masoko na Uenezi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Costantina Martin pamoja na
Mwanamitindo Flaviana Matata wakitoa mabegi kwa mmoja wa wanafunzi wa shule ya
Msingi Mnengulo mkoani Lindi. Jumla ya wanafunzi 650 wa shule zilizipo
katika Halmashauri za Lindi na
Nachingwea mkoa wa Lindi wamenufaika na
msaada huo wa mabegi hayo yenye vifaa mbalimbali vya shule, msaada huo
umetolewa kwa pamoja kati ya PSPF na Taasisi ya Flaviana Matata
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...