Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakwanza kushoto akiwa na Waziri wa Ujenzi
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.
Rehema Nchimbi pamoja na Mbunge wa Kongwa ambaye pia ni Naibu
Spika Job Ndugai wakifurahia mara baada ya Rais kuweka jiwe la Msingi
Ujenzi wa Barabara ya Mbande-Kongwa 16.5Km .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe
Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi, Mbunge
wa Kongwa ambaye pia ni Naibu Spika Job Ndugai, Makamu Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Profesa Juma Kapuya pamoja na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe, akikata utepe
kuashiria uzinduzi rasmi wa barabara ya Mbande-Kongwa 16.5Km.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akipiga ngoma pamoja na kikundi cha ngoma za asili cha Kibaigwa kabla
ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete kuhutubia mamia ya Wakazi wa Kibaigwa.
Sehemu ya barabara Mbande-Kongwa 16.5Km ambayo
ujenzi wake umewekwa jiwe la Msingi.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
kulia akizungumza na Mbunge wa Kibakwe ambaye pia ni Naibu Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa George
Simbachawene huku Mbunge wa Kongwa ambaye pia ni Naibu Spika Job
Ndugai akishuhudia kushoto.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
katikati akizungumza na Mbunge wa Kongwa ambaye pia ni Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job
Ndugai (kushoto) pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya
Miundombinu Profesa Juma Kapuya(kulia) kabla ya uzinduzi wa barabara
ya Mbande-Kongwa 16.5Km.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa
Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya uzinduzi na ufunguzi wa
barabara ya Mbande-Kongwa 16.5Km.
Viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Ujenzi pamoja na
Taasisi zake wakimsubiri Rais Dkt. Jakaya Kikwete kuzindua rasmi mradi
wa Ujenzi wa Barabara ya Mbande-Kongwa 16.5Km.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Ujenzi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...