Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu wa Maafa imesema itawatumia
Wataalam waliopo katika Ngazi ya Kata katika Mradi wa kuzijengea uwezo jamii wa
kuzuia, kupunguza na kukabiliana na maafa yanayotokana na ukame. Kauli mbiu ya
Mradi huo ni “Athari za Ukame Zinapunguzika, Jamii ikielimishwa.”
Akiongea wakati wa Mafunzo juu ya Utekelezaji wa Mradi huo kwa Wataalam wa
Sekta ya Kilimo, Mifugo, Afya, Elimu na Utawala wa kata ya Hedaru, Makanya na
Vunta, Wilayani Same, Mratibu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wa Mradi huo Bw. Harrison
Chinyuka alifafanua kuwa lengo la Mafunzo hayo ni kuwajengea Uwezo wataalam hao
wa kutambua viashiria na vihatarishi vinavyoweza kusababisha maafa ili waweze kutoa
elimu sawia kwa vikundi vinavyotekeleza mradi huo katika kata zao.
“Kutokana na mabadiliko ya Tabia Nchi yameleta athari nyingi ikiwemo ukame, kupitia
mradi huu ulioanza kutekelezwa kwa majaribio katika Wilaya ya Same hasa katika
Kata ya Hedaru, Makanya na Vunta, hivyo wataalam kupitia mafunzo haya wataweza
kuvieimisha vikundi vya kata zao husika juu ya kuzuia, kupunguza na kukabiliana na
maafa yanayotokana na ukame.” Alisema Chinyuka.
Chinyuka alifafanua kuwa Wataalamu hao katika ngazi ya kata ndio waratibu
katika kuijengea jamiii uwezo wa kukabiliana na kupunguza vihatarishi vinavyoweza
kusababisha maafa ya ukame kwakuwa Wataalam hao hutoa mafunzo kwa wadau
kuhusu matumizi ya mbegu na pembejeo za kilimo, mifugo na misitu pamoja na
upatikanaji wa maji safi na salama kwa matumizi ya binadamu na mifugo.
Wakitoa mada wakati wa mafunzo hayo Wakufunzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania na Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika
walibainisha kuwa Wataalam katika Sekta ya Kilimo, Mifugo, Afya, Elimu na Utawala wa
kata ya Hedaru, Makanya na Vunta wanalo jukumu la kuelimisha jamii juu ya matumizi
ya Taarifa za Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini pamoja na Umuhimu wa Tathmini ya Hali
ya Chakula na Lishe Nchini katika kata zao.
Akiongea wakati wa kufunga mafunzo hayo Afisa Mtendaji Kata Hedaru, Bw. Jackson
Mbwambo alibainisha kuwa mafunzo hayo yamewajengea uwezo wataalam wa ngazi
ya kata wa kuweza kupunguza athari za maafa ya ukame na kuahidi kushiriki kikamilifu
katika kuijengea jamiii uwezo wa kukabiliana na kupunguza vihatarishi vinavyoweza
kusababisha maafa ya ukame katika kata zao.
Mikoa ya Kilimanjaro na Shinyanga ndio inayotekeleza mradi huo, wilaya zinazoshiriki
katika mradi huo ni pamoja na Same, Hai na Mwanga kwa mkoa wa Kilimanjaro na
Wilaya za Kishapu, Shinyanga Vijijini na Shinyanga Mjini kwa mkoa wa Shinyanga.
Mradi Wa Kuijengea Jamii Uwezo Wa Kupunguza Athari Za Maafa Kwa Mikoa
Iliyoathirika Zaidi Na Ukame umefadhiliwa na Benki ya Dunia na kusimamiwa na
UNICEF chini ya Uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Halmashauri husika wakiwa
Watendaji Wakuu wa Mradi huo. Mradi huo unatekelezwa kwa kipindi
uliozinduliwa Wilayani Same, mkoani Kilimanjaro tarehe 11 Desemba2013.
Baadhi ya Wataalam katika Sekta ya Kilimo, Mifugo, Afya, Elimu na Utawala wa kata
ya Hedaru, Makanya na Vunta Wilayani Same, wakinukuu masuala muhimu wakati wa
mafunzo ya jinsi ya kutekeleza Mradi Wa Kuijengea Jamii Uwezo wa kupunguza Athari
Za Maafa katika kata zao, mafunzo hayo ya muda wa wiki moja yameratibiwa na Ofisi
ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu wa Maafa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...