Wakala wa Usajili,Ufilisi na Udhamini (RITA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) itafanya tathmini ya mfumo wa usajili wa matukio muhimu ya maisha na ukusanyaji wa takwimu nchini.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA,Bw. Phillip Saliboko  alisema Tathimini hiyo itafanyika kikanda kwa siku 15 kuanzia tarehe Septemba 15 - 30, 2014 na kujumuisha wadau wakubwa wa mambo ya usajili kutoka kwenye baadhi ya Wizara,Taasisi ,Idara Vyuo vikuu na Wakala wa Serikali huku ikijikita zaidi katika kuangalia matukio makuu manne ambayo ni vizazi, vifo na sababu zake,ndoa na talaka.

Matokeo ya tathimini hiyo itatumika kuisaidia Serikali kutekeleza mikakati yake ya kurekodi na kutunza taarifa hizo muhimu badala ya kutegemea Sensa peke yake ambayo hata hivyo huchukua muda mrefu kufanyika huku matukio hayo yakitokea kila siku na kuhitaji kufanyiwa kazi.

Jitihada za kuanzisha mfumo huo barani Afrika zilianza mwaka 2008 wakati Mh. Dkt Asha-Rose Migiro (Mb) Waziri wa Katiba na Sheria alipokuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa pia wakati huo akiwa kama Mwenyekiti wa Kikao cha tathimini ya malengo ya maendeleo ya milenia kwa kundi la Afrika.
Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA,Bw. Phillip Saliboko akitoa maelezo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo asubuhi kwenye Ukumbi wa Mikutani wa RITA,kuhusu Tathimini ya kuwezesha kupatikana kwa mfumo thabiti wa usajili wa matukio muhimu ya maisha na ukusanyaji wa takwimu.Kushoto Meneja wa Usajili wa Vizazi na Vifo,Bi.  Angela Anatory na kulia ni Meneja Masoko wa RITA,Bw. Josephat Kimaro.

Meneja wa Usajili wa Vizazi na Vifo,Bi.  Angela Anatory akizungumza na Waandishi wa habari katika Mkutano huo uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi za RITA,Upanga jijini Dar.Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA,Bw. Phillip Saliboko.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...