Happy-Siana Appia Kirenga
19.12.1966 - 5.07.2014
Familia ya Marehemu Mzee Appia Thomas Kirenga wa Machame Kisiki
Moshi inayo heshima kubwa kutoa shukrani za dhati kabisa kwa ndugu, jamaa na
marafiki ambao walishiriki kwa namna moja ama nyingine kufanikisha msiba,
mazishi na hatimaye matanga ya mtoto/Dada yao mpendwa, Happy-Siana Appia
Kirenga aliyefariki dunia usiku wa Jumamosi
ya July 5 kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kuzikwa jirani na alipopumzishwa
baba yake mzazi, nyumbani, Alhamisi ya July 10, 2014.
Kwa vile walivyotuunga mkono na kutufariji wakati wa kipindi
hiki kigumu cha msiba huu mkubwa ni wengi na ni vigumu kuwataja wote kwa
majina, Familia, inapenda kwa heshima na taadhima nyingi kutoa shukrani za
jumla ikiwaomba wote mkubali kuzipokea kwa moyo ule ule kama mlivyotuunga
mkono. Mmetufariji sana, mmekesha nasi, mmeshinda nasi, nyote mmekuwa kimbilio
salama kwetu wakati wa kipindi hiki kigumu.
Mmeonesha upendo wa kweli kweli kwetu kama Familia na kwa
mwanetu dada yetu ambaye angerejea kwenye uzima tena, naye bila shaka yoyote
angetoa shukrani za dhati ya moyo wake.
Hata hivyo, tunapenda kutoa shukurani kwa makundi machache ya marafiki ambao
mchango wao utabakia kwenye nyoyo za wazazi na familia yetu tukianza na majirani na marafiki wa karibu wa
Familia walioko Dar es Salaam, Moshi, Arusha, Morogoro, Dodoma, Manyara, Kagera,
Mbeya na kwingineko Tanzania, Kenya na nje ya Afrika Mashariki, ambao michango
yao kamwe haitasahaulika.
Familia pia inapenda kuwashukuru wanajumuia wa Sayuni Mtaa
wa Neema Usharika wa Mbezi Makabe Dar Es Salaam, Uongozi na Washarika wa
Makongo Juu Dar es Salaam, uongozi na Washarika wa Kalali Machame Moshi na
Watumishi Wengine wa Mungu kutoka sharika mbalimbali wakiongozwa na Askofu
Mstaafu Dk Erasto, N. Kweka kwa huduma
kubwa za kiroho wakati wa msiba huo mkubwa uliotufika.
Familia vile vile inapenda kutoa shukrani za dhati kabisa
kwa Dr Ayoub Pamba, na kwa Wauguzi na Madaktari wa Hospitali za Tumbi Kibaha na
Muhimbili Dar es Salaam kwa juhudi zao za dhati za kutaka kuokoa maisha ya Dada
yetu
Aidha, tunatoa shukrani kwa wafanyakazi na uongozi wa Super
Sky Aviation, Regional Air Limited,
Wafanyakazi marubani wakiongozwa na Kapten Tatiya Tukero Naikuni, na mfanyakazi
mmoja mmoja kwa jumla michango yenu, ilitufariji na tutaendelea kukumbuka
ukarimu wenu daima.
Vile vile, Familia inawashukuru sana wanakijiji cha Wari, Kata ya Machame,
Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro, kwa kuupokea vizuri na kuushughulikia kwa
heshima zote msiba wa mtoto wao Happy-Siana Appia Kirenga.
Mwisho
Tunawashukuru nyote mlioweza kufika nyumbani Machame Kisiki kumhifadhi Dada
Happy. Hatuna cha kuwalipa, Mungu
atawalipa.
“Mathayo 5: 8 :- Heri wenye moyo safi; Maana
hao watamwona Bwana”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...