Na Greyson Mwase, Bagamoyo
Imeelezwa kuwa Tanzania inatarajia kuwa kitovu kikuu cha madini ya vito barani
Afrika baada ya kubainika kuwa na utajiri mkubwa wa madini ya vito.
Hayo yalisemwa na mtaalamu wa madini ya vito na almasi kutoka Kitengo cha
Uthamini wa Madini ya Vito na Almasi (TANSORT) kilicho chini ya Wizara ya
Nishati na Madini Teddy Goliama kwenye semina iliyoshirikisha Makamishna
Wasaidizi wa Madini wa Kanda, Afisa Madini Wakazi na Wataalamu kutoka Wizara
ya Nishati na Madini inayoendelea mjini Bagamoyo.
Goliama alisema Tanzania kupendekezwa kuwa kitovu kikuu cha madini ya
tanzanite ni matunda ya ziara iliyofanywa na Kitengo cha TANSORT kwa
kushirikisha wataalamu wa wizara ikiwa ni pamoja na ushiriki wake katika
maonesho ya kimataifa ya vito ya Thailand yajulikanayo kama Bangkok Gem and
Jewellery Fair.
Alisema sababu zilizopelekea Tanzania kupendekezwa kuwa kitovu cha biashara
ya madini ya vito Afrika ni kutokana na wingi na aina mbalimbali za madini hayo
pamoja na madini hayo kupendwa na wafanyabiashara wengi kutoka Thailand na
nchi nyinginezo duniani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...