Na Rose Masaka-MAELEZO
Umoja wa Wapiganaji wa Sanaa ya Mapigano Duniani (UPAM) unaandaa shindano la kimataifa la wapiganaji ambalo linatarajiwa kufanyika nchini kati ya Mwezi Desemba mwaka huu na mwanzoni mwa mwaka ujao kutokana na ruhusa itakayotolewa na Serikali kwa mamlaka zinazohusika.
Kauli hiyo imetolewa leo na Rais wa UPAM Prof. Maurizi Mardina alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam
Profesa Mardina amesema kuwa mchezo wa kupigana ni mchezo mzuri ambao unahitaji kujitoa na uwezo mzuri wa kufikiri na siyo mchezo au mafunzo yanayosababisha uonevu bali ni mafunzo yanayompa mtu uwezo wa kujilinda na kujitetea.
Ameongeza kwa kusema kuwa Nchi 102 zinatarajiwa kushiriki mashindano hayo ambapo watashiriki wachezaji 25 wa umri na jinsia zote kutoka katika nchi hizo.
“Walimu wanafundisha vizuri ili kuandaa timu bora na baadhi ya vifaa tayari vimenunulia vyenye thamani ya dola ya kimarekani 25000.” amesema Mardina.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa UPAM Tanzania Joe Jolamu ameeleza kuwa mashindano ya ndani tayari yameishaanza na yanaendelea ili kuweza kupata timu moja ya taifa itayocheza katika mashindano ya dunia.
“Wachezaji ambao wataruhusiwa kujiunga na kuingia katika kuchezea timu ya dunia ni wale tu ambao wapo katika kikosi maalumu” alisema mwalimu Jolamu.
Aidha, mmoja wa wanafunzi wa mchezo huo Hafidhi Kunambi anayepata mafunzo ya mchezo huo ameonesha jinsi alivyojifunza namna ya kujilinda kadiri ya mafunzo aliyopata.
Kwa Tanzania wanatakiwa washiriki 45 ambao wamefanya mazoezi ili kuweza kushiriki mashindano hayo kutoka maeneo mbalimbali nchini na kupata timu bora itakayoleta ushindi.
01. Katibu
Mkuu wa UPAM Tanzania Joe Jolamu (kushoto) akingea na waandishi wahabari leo
jijini Dar es salaam juu ya mashindano ya karate ya dunia yanayotarajiwa
kufanyika nchini mwishoni mwa mwaka huu au mwanzoni mwakani. Kulia ni Rais wa
UPAM duniani Prof. Maurizi Mardina.
01. Rais
wa UPAM duniani Prof. Maurizi Mardina akimshikilia shingo Master Hudu Thabit
akionesha moja ya mbinu inazotumika kwa kujihami kwa ajili ya usalama.
01. Rais
wa UPAM duniani Prof. Maurizi Mardina (kushoto) baada ya kuonesha mbinu ya
kujihami kwa mwandishi wa habari Kibwana Dachi (aliyekaa). Kulia ni Master Hudu
Thabit.
(Picha
zote na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...