Katika kuadhimisha miaka 100 ya kuanza kwa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, Tanzania,
Ubelgiji, Ugiriki, Iraki, Kenya, Nigeria na Afrika Kusini zimeungana na India katika
hafla iliyoendana na uzinduzi wa kitabu cha picha za kumbukumbu za wapiganaji
waliofariki kwenye vita hiyo kuanzia mwaka 1914 – 1918.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, iliyofunguliwa na Mhe. Ban Ki-moon, Katibu Mkuu
wa Umoja wa Mataifa na Mhe. John W. Ashe, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
na kuhudhuriwa na Wawakilishi wa nchi mbalimbali Wanachama wa Umoja wa Mataifa,
Mhe. Ramadhan M. Mwinyi, Kaimu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania amesema
kitabu hicho ni mchango muhimu katika historia ya vita hivyo, vilivyosababisha maafa
makubwa katika mabara ya Ulaya, Asia na Afrika, ambapo jumla ya watu milioni 16
walifariki dunia na wengine milioni 20 kupata majeraha makubwa.
Balozi Mwinyi alitumia fursa ya hafla hiyo kuikumbusha jumuiya ya kimataifa, wajibu
wa kizazi cha sasa, kuendelea kusisitiza umuhimu wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya
mazungumzo kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mwaka
1945.
Akizungumza kwa hisia kali, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alisema hata baada
ya athari kubwa za Vita Kuu mbili za Dunia, Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa
hazijajifunza umuhimu wa kuepusha vita na migogoro. Matokeo yake, dunia imeendelea
kugubikwa na migogoro mbalimbali ambayo imesababisha vifo, majeruhi, uharibifu
mkubwa wa miundo mbinu na mazingira.
Naye Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa alihoji kama Vita hivyo vilipaswa
kuitwa Vita Vikuu, badala yake alisema vingeitwa Janga Kuu la dunia. Rais huyo
alisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa nchi zote za Umoja wa Mataifa katika kuzuia na
kutatua migogoro.
Tanzania bara, wakati huo ikiwa chini ya himaya ya wakoloni wa Kijerumani, iliguswa
na vita hivyo vilivyopiganwa na watawala wa Kijerumani na Waingereza katika maeneo
ya Afrika Mashariki. Inakadiriwa kuwa, wanajeshi na raia takriban elfu hamsini wa
eneo hilo walipoteza maisha katika vita hivyo. Miongoni mwao ni wanajeshi wa Kihindi
ambao walipigana upande wa Waingereza. Minara ya kumbukumbu pamoja na makuburi
ya wanajeshi hao ipo Dar es Salaam, Taveta naTanga.
Tanzania ilisisitiza kuwa, ni vyema kuwakumbuka wengine wengi ambao walipoteza
maisha wakati na baada ya vita, kutokana na maradhi na njaa. Pia ilitaja maeneo mengine
ambayo ni kumbukumbu ya vita hivyo kama vile sanamu ya askari (Askari Monument)
iliyopo katikati ya jiji la Dar es Salaam na Kariakoo, ambako waliishi wanajeshi wa
Kihindi waliojulikana kwa Kiingereza kama “Carrier Corps”.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwa na Wawakilishi wa Nchi zilizoandaa hafla hiyo.
Mhe. Ramadhan M. Mwinyi, Kaimu Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwasilisha hotuba yake kwenye hafla hiyo.
Wakati wa ujerumani hakuna kitu kinachoitwa "tanzania bara'; tuseme ukweli ni "Tanganyika". Siye Waswahili tuna msemo wetu, mficha uchi hazai. Kwa hiyo Tanganyika ndiyo iliyokuwa kipindi hicho na ipo hadi leo; ndiyo maana tunasherehekea uhuru wetu kila ifikapo Disemba 9 kila mwaka. Tuwafundishe vyema historia watoto wetu na wajukuu zetu. Wanasemaga asiyejua anakotoka hatojua anakokwenda. Kazi njema kaka michuzi.
ReplyDeleteSomething should be wrong somewhere.....!!
ReplyDelete