KAMPUNI ya Tanzania Distilleries Ltd (TDL) imeendelea kujitanua katika soko nchini baada ya kuzindua kinywaji kipya cha kimataifa kiitwacho Fyfe's Scotch Whisky.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kinywaji hicho Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa TDL, David Mgwassa alisema Fyfe's ni kinywaji maridhawa kinachoandaliwa kikamilifu kikiwa na radha murua na ya kipee.

"Ubora wa kinywaji hiki unatokana na umahiri mkubwa wa waandaaji na pia unatokana kimea na nafaka bora zilizotumika na kuwa Fyfe's Whisky huvundikwa kwa miaka kadhaa katika mji Loch Lomond, Scotland ili kuongeza ubora wake kabla ya kuwa tayari kwa matumizi" alisema Mgwassa.

Mgwasa aliongeza kuwa kampuni yao imekuwa ikiwaletea watanzania vinywaji mbalimbali ambavyo vimekuwa chachu katika kusherehekea hatua tofauti za mafanikio yao na kuendelea kuwaletea ladha tofauti za vinywaji bora.

Alisema kinywaji hicho ni zawadi ya pekee katika soko na kuwa Tanzania imekuwa nchi ya kwanza ulimwenguni kuzinduliwa na baadaye kitazinduliwa nje nyingine.
Mkurugenzi Mtendaji wa TDL, David Mgwassa, akizungumza na wadau mbalimbali wakati wa hafla ya uzinduzi wa kinywaji hicho.
Langa Khanyile akitoa ufafanuzi wa Whisky hiyo kabla ya uzinduzi.
Sehemu ulipo fanyika uzinduzi huo katika Hoteli ya Serena.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd (TDL), David Mgwassa (wa pli kushoto), akiwa na baadhi ya wageni waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa kinywaji kipya kiitwacho Fyfe’s Scotch whisky, iliyofanyika Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL), Kushila Thomas.

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...