Suala la hivi karibuni la nchini Israel la kiusalama mitandao linaloweza kusomeka "HAPA", Polisi wanchi ya Botswana kuonyesha wasi wasi wao juu ya maswala ya usalama mtandao kama inavyoweza kusomeka "HAPA" pamoja na matukio mengine kadhaa ya uhalifu mitandao ambayo yamekua yakigonga vichwa vya habari hivi sasa yameibua swali, je kuna uwezekano mapambano dhidi ya uhalifu kufikiwa malengo kwa kupunguzwa walau kwa kiasi Fulani?
Jibu ni kwamba hivi sasa uhalifu mtandao umeendelea kukua huku pakitumika njia za kisasa na hatarishi zinazo onekana kua tishio katika mifumo ya mitaandao katika nchi nyingi duniani. Ingawa pia wataalam wa maswala ya usalama mitandao wameendelea kujipanga na kuangalia kila namna ya kuweza kukabiliana na uhalifu mtandao katika ngazi ya kidunia.
Kubwa lililo jiri hivi karibuni kumeendelea kutafutwa mbinu za kuhakiki uhalifu mitandao unapata kudhibitiwa huku baadhi ya makampuni nanchi mbali mbali kuchukua hatua stahiki nikitolea mfano "FACEBOOK" na tukio la "UJERUMANI" ikiwa ni mifano miwili kwa uchache.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...