Ndugu zangu Watanzania nafasi tuliyonayo sasa ni muhimu tukaitumia vizuri ili kuandika katiba yetu upya ili kukidhi matakwa ya sasa na vizazi vijavyo.

Nchi yetu ina bahati kupata viongozi wasikuvu na wenye nia njema na Taifa letu na ndio maana Mhe. Rais Kikwete alikubali hoja ya kuandika upya katiba licha ya kwamba haikuwa kwenye ilani wala vipaumbele vya Chama Cha Mapinduzi.

Na CCM kwa kuwa nia yake ni njema kwa Watanzania na ndio maana ikaridhia na mchakato ukaanza kwa utaratibu uliokubalika na wadau wote na ikatungiwa sheria.

Sheria hiyo ndio inayofuatwa ambayo ilihitaji uundwaji wa tume ikusanye maoni kwa wananchi na kutengeneza rasimu ya katiba ambayo itawasilishwa kwenye bunge maalumu la katiba (BMK) ili rasimu ile ijadiliwe na hatimaye BMK litoe rasimu ya mwisho itakayopelekwa kwa wananchi ili uamuzi wa mwisho ufanywe na wananchi wenyewe kama wanaikubali au wanaikataa hiyo rasimu iliyopitishwa na BMK.

Sasa hapa kinachonishangaza ni kuwa kama tulikubali uteuzi wa BMK na mjadala ukaanza kwa nini katikati ya mjadala baadhi ya watu wanasusia ? Kwa nini wasiendelee na mjadala na wakashindana kwa hoja ? Je ni kweli watu hawa wana nia njema na Taifa letu au wana maslahi fulani ila wanatumia hii kama sababu ?

Mimi kama mwamnamichezo huwa kabla ya kuanza mchezo tunakubaliana kanuni, taratibu na sheria itakayotumika katika mashindano husika na mkishaanza timu moja katikati ya mchezo inasusa ni dhahiri timu hiyo inapoteza sifa za uanamichezo na matokeo yake ni kutoa ushindi mwepesi kwa mshindani wake.

Kama kweli kundi hilo lilikuwa linataka katiba basi warudi kwenye uwanja wa majadiliano na watoe hoja na hatimaye mwenye hoja yenye mashiko atashinda lakini wakumbuke wenye uamuzi wa mwisho ni wananachi na sio wajumbe wa BMK. Hivyo basi uamuzi wowote utakaopitishwa bado sio wa mwisho bado kuna nafasi ya kuamua kwa maslahi ya Taifa.

Kuhusu rasimu ya tume ya Warioba, mimi nadhani Watanzania tuwe wakweli naomba nitumie mfano wa kikao cha sherehe za kawaida (mf. Harusi) mnapokutana kundi kubwa kujadili namna ya kufanikisha sherehe ile hamuwezi kundi lote kukubaliana kila kitu na pengine mnaunda kamati ndogo ya kutengeneza mambo muhimu kama bajeti, ratiba n.k sasa kamati ndogo inatengeneza rasimu ya bajeti kulingana na maoni ya baabhi ya watu na kamati ile inaleta rasimu ya bajeti kwenye mkutano mkubwa wa sherehe na mkutano ule unaamua kukubali baadhi ya mapendekezo, mengine kuyaboresha, mengine kuyabadili na mengine kuyakataa. Sasa baada ya hapo kinachokubaliwa na mkutano huu ndicho cha wote na wote tuna wajibu wa kukitekeleza kwa mujibu wa makubaliano.

Sasa kwa BMK kuboresha mapendekezo ya tume ya Warioba kuna tatizo gani ? Kila kipengele cha rasimu kimejadiliwa na kutolewa mapendekezo, vingine vimekubaliwa, vingine vimeboreshwa na vingine havijakubaliwa sasa hapa tatizo ni nini mbona ni utaratibu wa kawaida kwenye taratibu za mikutano ? Kama nilivyoeleza hapo juu.

Cha ajabu hapa nini ? Labda tueleweshane, tume ya Warioba imefanya kazi yake imemaliza, sasa hatua inayofuata ni BMK nalo linapokea rasimu linajadili na linatoa rasimu yake ambayo ndio itaamuliwa na wananchi.

Hivi tulitarajia kila kilichopendekezwa na tume ya Warioba kipite kama kilivyo ? Sasa kazi ya BMK ni nini ? Mbona hata katika Bunge la kawaida Serikali au Mbunge yoyote analeta hoja na hoja ile inajadiliwa na hatimaye inapitishwa kama ilivyo au inapitishwa na marekebisho au inakataliwa na mwisho wa siku uamuzi wa Bunge baada ya majadiliano ndio unaheshimiwa.

Sasa kwa nini leo baadhi ya watu wanataka kutuaminisha eti kila kilicholetwa na tume ya Warioba ndio sahihi, kama ni hivyo basi sheria ingesema baada ya tume kukusanya maoni, maoni yale kama yalivyo yapelekwe kwa wananchi kwa uamuzi. Lakini sheria iko wazi na ndio inayofuatwa sasa kwa nini leo watanzania tunataka kuvunja taratibu tulizojiwekea wenyewe ?

Kama unakwenda kwenye majadiliano na wewe unasema lazima hoja yako ndio ipite basi bado hujakomaa na hujui hata taratibu za majadiliano. Inabidi kwanza uelimishwe ili uwakilishi wako uwe na tija, vinginevyo utapoteza rasilimali za watu bure na mwisho kusiwe na tija.

Kitendo cha kususa hakina faida kwa Taifa wala kwa wananchi/makundi wanayowakilisha.

Ni muhimu tuwe na wanasiasa wenye ukomavu wa kisiasa na wenye kuweka mbele maslahi ya Taifa na sio maslahi binafsi.

Ni muhimu tujue kuwa kwenye mchakato wowote kuna kupata na kukosa hivyo viongozi na wawakilishi wetu wawe tayari kwa yote.

Nashauri wale wote waliosusa BMK kurejea kwenye majadiliano kwenye BMK na watoe hoja zao humo na wenye hoja zenye mashiko watashinda na hatimaye watuletee rasimu tutakayoamua sisi wananchi.

Phares Magesa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. One important clarification, Warioba Commission was tasked to draft Raskku based input from the people. Your metaphor "Vikao vya harusi" does not necesssarily apply to this case. Asante kwa hoja.

    ReplyDelete
  2. Kinacholeta shida ni muundo wa serikali 2 ama 3. Kwa nini hawa wajumbe wa BMK wasijadili faida za serikali 2 na 3, hasara zake, pia waje na case studies na mifano halisi ya serikali 3 au zaidi ambazo hatujawahi kuwa nazo hapa TZ ili wakubaliane. Shida ninayoiona pengine wale walio tayari na uongozi wanashindwa kufanya hivyo kwa kuwa kila mtu anataka awe kiongozi. Yaani ni kwamba "haiwezekani" kila mtu kuwa kiongozi lazima tuwe na viongozi wachache tu waliochaguliwa na wananchi. Hivi ninyi mnaobishana na kushindana hamjui hilo??? Hebu onyesheni ukomavu jamani sisi tumechoka kusikiliza yenu hayo ya kila siku. Hivi serikali za Afrika mkoje, hadi Wazungu waje kuwaamulia mambo yenu? ..duh!!!

    ReplyDelete
  3. Nashangaa sana..hii katiba si yetu peke yetu ni ya vizazi vijavyo pia, yaani watoto na wajukuu zenu hivi hamuelewi? Miaka 100 ijayo mwisho wa mkataba wa gesi nyote ninyi hamtakuwapo duniani..hivi hamuelewi Watanzania? Mbona mnawaza maslahi yenu? Mnataka kurithisha uongozi na mali za ufisadi? Sasa muache selfishness. .fanyeni kazi ya wajukuu wenu. Hamjasikia mnaambiwa 'msikate miti ovyo ni ya wajukuu wenu, hamuelewi" mnaambiwa msiingie mikataba feki itawaathiri wajukuu zenu, hamtaki, enyi kizazi kilicholaaniwa..nani kawaloga? Hivi wajukuu zenu si watakutana na majanga baada ya miaka kibao..yaani ninyi watz naona mmelogwa kabisa. Mnamlaani baba wa taifa..mbona wachina wanawatukuza akina Mao..india akina Gandhi..Tanzania mtalaaniwa..ohooo! Au hamjui mmemwacha Mungu?Kwa kweli Mungu awaonyeshe cha kufanya..wote waliomwacha Mungu wamepotea! Shauri yenu akina Tundu Lissu mnaendelea kutumia akili zenu! Imeandikwa na alaaniwe ategemeaye akiki zake mwenyewe! Mwana mutuka liso panse...!

    ReplyDelete
  4. Ikiwa mtu kama huyu msomi mzuri na mwenye wadhifa mkubwa huu ndiyo msimamo wake , shida ni kubwa sana.

    ReplyDelete
  5. Wow this article is a joke,really you gotta compare a wedding committee and a committee assigned to collect peoples wwishes?

    ReplyDelete

  6. KAKA MAGESA UMECHEMKA! mambo ya "VIKAO VYA HARUSI" vinavyofanywa wakati watu wanakunywa pombe na nyama choma ni kinaweza kulinganishwa na kikao muhimu cha katiba?
    najua wana CCM mpo kwenye PR na kampeni ya propaganda ya kufanikisha
    "KATIBA YA CCM" MTAWEZA KUIPATA HIYO KATIBA ILA ITAKUWA YA MUDA...
    KWANI HAITAKUWA YA WOTE.. ITAKUWA YA CCM.
    NAJUA MABADILIKO YA HAKI NA UKWELI KUPITIA KATIBA HAYAJI KIURAHISI...
    UKAWA WAMEONA HILO KUWA UANDAAJI KATIBA YA HAKI KWA WOTE NA YA UKWELI HAUENDI KI HAKI NA UKWELI, SULUHISHO NI KUPIGANA NDANI AU NJE UKUMBI....
    TUKUBALI AU USIKUBALI KAKA MAGESE, UKWELI WOTE TWAUJUA.... KATIBA MPYA YENYE MAFAO KWA WATZ WOTE HAIPATIKANI KWA AJILI YA CCM PEKE YAKE AU UKAWA, KUBALINI KULA "VIDONGE" VYA TUME YA WARIOBA.... KNA KAMWE MSIDHANI MTAONGOPOEA UMMA KWA HILI... WATZ TUMEAMKA THIS TIME...TWAJUA HAKI ZETU...

    ReplyDelete
  7. Eh Hays undo msoni ya kiongozi kijana wa CCM anayesubiri uongozi! Mungu mlaze pema marehrmu Wakili Mages a baba take Phares,angrsikia Hays main I name utalaamu wake ea she ria kwamba katiba inalinganishwa na vikao vya send off, angekukana hadharani

    ReplyDelete
  8. Watz ni watu wa maajabu kweli. Yote ya maana aliyozungumza hamkuyaona ila vikao vya harusi. Someni hoja, jibuni hoja. Msifanye mambo kiujumla. Rasimu imeandaliwa iende Bungeni kujadiliwa. Hata Warioba sio malaika pamoja na Tume yake. Tuchambue mazuri, yasiyofaa yaachwe. UKAWA hawana hoja. Kwanini walichangia chapter 1&6? Z

    ReplyDelete
  9. KATIKA HADI YOYOTE LAZIMA TUKUBALI CCM WAKO WENGI KATIKA HALI HIYO LAZIMA UKAWA MJIPANGE NA MJIULIZE MNAUNGWAJI MKONO KIASI GANI NI KWELI HADI VIJIJINI WANAWAELEWA? HUKO NDIKO CCM KUNAPOWAFANYA WAWE JEURI JIPIMENI TAFITI ZINAWAKUBALI?,VIPI MATOKEO YA 2010? MTAJAZA WATU LAKINI MUULIZENI MREMA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...