Napenda kuwajulisha kwamba mtoto Faith amepatikana maeneo ya Msasani na ameshaungana na familia. Aliokotwa na Msamaria mwema ambaye nae alikuwa anafanya juhudi za kuitafuta familia yetu.

Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru sana sana kwa msaada wenu wa kurusha habari ile ya kupotea kwake. Lakini zaidi sana nawashukuru  jinsi mlivyotenda kwa haraka (act promptly) nilipotuma tu ujumbe.

Hii imeonyesha umuhimu wa mitandao hii na ni kweli ya wananchi na jamii. 

Asanteni sana na kila la heri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mungu apewe sifa kupatikana mtoto huyu, wazazi na walezi angalieni watoto wenu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...