Mahmoud Ahmad,Arusha
Timu ya Ushirika Veteran ya mkoani Kilimanjaro imeibuka bingwa wa Bonanza la Nanenane kwa kuifunga timu ya Kivule veteran ya ukonga jijini Dar es salaam kwa magoli 3-0  katika mchezo wa fainali ya mashindano hayo yaliondaliwa na timu ya Arusha All Stars kwenye uwanja wa sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Michezo hiyo ya nanenane iliyozishirikisha timu kutoka mikoa ya Arusha,Dodoma, Mwanza,Dar es salaam na Kilimanjaro ambao timu yao ndio waliibuka mabingwa wa mashindano hayo kwa timu za ushirika veteran na kivule kucheza fainali

Hata hivyo wenyeji wa mashindano hayo waliambulia nafasi ya nne baada ya kufungwa katika mechi ya kugombea nafasi ya tatu na timua ya Dodoma veteran iliyokuwa inaongozwa na mkongwe wa soka hapa nchini Charles Mgodo.

Akizungumza baada ya mechi hiyo mgodo aliwataka wachezaji wa sasa kuangalia michezo ya maveterani katika mabonanza mbalimbali kwani watajifunza kitu kutoka kwao ikiwemo nidhamu ya michezo na kujituma kama walivyoonyesha baadhi ya wachezaji wa miaka ya nyuma wa timu zilizotamba kwenye ligi kuu.

Pia Mgodo alisema kuwa maandalizi ya timu za vijana wa sasa na wazamani ni tofdauti huku akisema kuwa vijana wa sasa wanataka kucheza kama mchezaji Fulani baada ya kuangalia tv huku hawajitumi hili ni tatizo na kuwataka kuanza kujituma na kutoweka maslahi mbele na kuuvaa uzalendo.

Akalishauri shirikisho la michezo hapa nchini Tff kurudi mashuleni au kuanzisha Academy ilkuweza kuibua vijapaji na sio kuviacha vikielea bila ya kuviendeleza hili ni tatizo kwa ukuaji wa michezo hapa nchini.

“Tunataka vijana wakija kwenye mabonanza waje kujifunza mpira na kuangalia tofauti ya mpira wanaocheza wao na wa wazee wao hapa umeona wachezaji wa zamani wakijituma tokea mwanzo wa mchezo hadi mwisho na wao wanatakiwa kuwa kama hivi ila kikubwa wawe wazalendo kwa taifa lao hapo tutafanikiwa”alisema Mgodo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Katika habari hiyo, tunaomba angalau ututajie majina ya wachezaje wa Ushirika Veterani waliocheza mechi hiyo.Tutafarijika sana na itatukumbusha enzi timu hiyo ilipokuwa katika kiwango kizuri cha soka nchini chini ya Mwl. Dan Korosso.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...