Kampuni ya Vodacom imerekebisha mfumo wa M-Pesa kwa soko la Afrika Kusini ili kuleta mafanikio kama yaliyopatikana katika nchi za Kenya na Tanzania.

M-Pesa ilianzishwa Kenya mwaka 2007 na leo hii inatumiwa na watu zaidi ya  milioni 18 katika nchi zipatazo 13 kwa ajili ya kutuma pesa na za kibenki kwa kutumia simu ya mkononi.M-Pesa ilianzishwa Afrika ya Kusini mwaka 2011 ikiwa na wateja wa mwanzoni zaidi ya milioni moja lakini hadi leo haijaonyesha kukua kwa soko kama ilivyo kwa nchi za Kenya na Tanzania,taarifa kutoka ndani ya kampuni zimeeleza.

Taarifa zimeendelea kueleza kwamba kutoka kipindi cha miaka miwili iliyopita Vodacom Afrika ya Kusini, imeunda jopo jipya la kushughulikia huduma ya M-Pesa na kuingiza utaalamu wa kutoka nje kuhusu shughuli za benki na malipo kwa njia ya simu,pia kuangalia ni mambo gani yamesababisha huduma hiyo kuzorota Afrika ya Kusini na kuangalia mafanikio katika nchi nyingine yametokana na nini.

Kutokana na tathmini iliyofanyika huduma mpya ya M-Pesa imezinduliwa ikiwa na marekebisho katika maeneo manne yakiwemo usambazaji,usajili,matumizi na imani katika mfumo wa M-Pesa.

Kuhusu usambaji,huduma mpya ya M-Pesa imeanzishwa kwa kuwa na mawakala wapatao 8,000 kukiwemo wadogo wadogo na mawakala wakubwa “idadi hii ni zaidi ya mara 10 ikilinganishwa na mawakala waliokuwepo wakati M-Pesa ilipozinduliwa Afrika ya Kusini mwaka 2011 na lengo ni kukua hasa katika sekta isiyo rasmi ili kufikia angalau mawakala 30,000 ifikapo mwisho wa mwaka huu”.Alisema Shameel Joosub,Mtendaji Mkuu wa makampuni ya Vodaccom Afrika Kusini.

‘’Upanuzi huu utatuweka mbele ya wengine katika shughuli za usambazaji kwa kuhakikisha kuna wakala wa M-Pesa kwa kila mita zisizozidi mamia mengi kutoka walipo wateja na pia kutakuwepo na ongezeko la ajira”.Aliendelea kueleza Joosub.

Kwa upande wa usajili M-Pesa ya Afrika Kusini imerekebisha taratibu za usajili kusudi wateja wajisajili kwa kutumia simu ya mkononi na kitambulisho tofauti na hapoo mwanzo ambapo mteja alilazimika kwenda mwenyewe kwenye kituo wakati vituo vya mawakala vilikuwa vichache.Kwa wateja wanaopenda  kubadili matumizi na kiwango cha kutuma fedha katika akaunti zao,wanachohitaji ni kwenda na vitambulisho vyao na kujisajili katika vituo maalumu zaidi ya 1,000 nchini vikiwemo maduka ya Vodacom,maduka mengine maalumu na vituo vingine vinavyohusika.

“Ingawa usajili na usambazaji ni muhimu lakini kubwa zaidi ni matumizi ya M-Pesa na tunafurahi kuona kwamba tumeshirikiana na benki ya Bidvest  inayotoa huduma za Visa vilevile ambayo imetupatia ushauri tukafanya marekebisho makubwa katika mfumo wa matumizi “Amesema Joosub.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa benki ya Bidvest Japie van Niekerk,   amesema kuwa taasisi yake inajivunia kufanya kazi na taasisi kubwa ya Vodacom katika kutoa huduma za kibenki kwa wananchi na ana imani wananchi watanufaika na huduma zitakazotoolewa kwa kutumia wataalamu wa taasisi yake na Vodacom.

Aliongeza kwamba ana imani kubwa kutokana na mabadiliko haya ya kuboresha huduma za M-Pesa wananchi wengi watafaidika na huduma hii ambayo tayari imerahisisha maisha kwa mamilioni ya wananchi wanaoutumia kutumiana pesa na kupata huduma mbalimbali katika nchi mbalimbali za Afrika mojawapo ikiwa ni Kenya na Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...