Wabunge wa EALA wakiwasili The Guardian Ltd
Wabunge wa EALA wakipokea maelezo kutoka kwa mfanyakazi wa EATV na Radio walipotembelea vyombo vya Habari vya IPP jana
Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Dkt Margaret Zziwa akizungumza baada ya kupokea maelezo kutoka kwa mfanyakazi wa EATV na Radio wakati wa Ziara ya wabunge hao IPP Media. Wa nne kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Joyce Mapunjo.
Wizara
ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuwataarifu wananchi kuwa Bunge la
Afrika Mashariki litafanyika kuanzia Agosti 27 hadi Septemba 4 katika ukumbi wa
Karimjee Jijini Dar es Salaam.
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kulihutubia Bunge hilo siku ya ufunguzi
Agosti 27.
Vikao
vya Bunge hilo vitakua vikifanyika kuanzia saa 8.30 mchana siku za Jumanne,
Jumatano na Alhamis.
Pamoja
na Mambo mengine Bunge hilo litajadili Muswada wa Elimu ya Mtangamano wa Jumuiya
ya Afrika Mashariki wa 2014 na pamoja na mambo mengine litapokea na kujadili
ripoti mbalimbali.
Wizara inawakaribisha wananchi
kufuatilia kwa karibu vikao vya Bunge la Afrika Mashariki ili waweze kujua
mambo mbalimbali yanayohusu mtangamano wa Afrika Mashariki.
Imetolewa
na:
KATIBU MKUU
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...