Na Mahmoud Ahmad,Arusha. 
 Vijiji 120 vilivyopo mkoa wa Arusha vinatarajia kufikiwa na huduma ya umeme kupitia mpango wa kusambaza umeme vijijini unaofadhiliwa na (REA) na kutekelezwa na shirika la umeme la taifa (TANESCO). 
 Benedict Nkini akizungumza katika mkutano na Wananchi wa Vijiji vya Meserani juu na chini amesema kuwa kwa sasa wako katika hatua ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya mradi huo ili waweze kujiandaa kuunganishwa na huduma hiyo na pia amewataka waepuke vishoka ambao hutumia uelewa mdogo wa wananchi kujinufaisha. 
 Afisa Masoko wa Tanesco,Adelina Lyakurwa amesema kuwa amewaomba wananchi kutumia fursa hiyo kuunganishiwa umeme huo wa bei nafuu ambao Mtanzania wa hali ya chini anaweza kuumudu ,ambapo Mwanakijiji atatakiwa kuwa na kiasi cha shilingi 32900 ili aweze kuunganishiwa umeme.
 “Tunawaunganishia umeme watu wote wenye nyumba za mawe,matofali,mbao kwa hiyo tunawaomba wananchi watoe ushirikiano ili kufanikisha mradi huu,kwa upande wa nyumba za nyasi na makuti kunahitajika ushauri wa kitaalamu kwasababu za kiutaalamu ili kuepuka moto ambao unaweza kutokea kutokana na hitilifu ndogo” Alisema Afisa Masoko huyo.
 Kaimu Mkurugenzi wa TANESCO wilaya ya Monduli ,Ramadhani Mkayala amewataka wananchi watafute wakandarasi wazuri waliodhinishwa na shirika ili kuepuka vihatarishi vya moto Kwa upande wao wananchi wa Wilaya ya Monduli Sophia Mligo wa kijiji cha Miserani na Gasper Lengta wamesema kuwa wameupokea mpango huo vizuri na kuwaomba TANESCO wazidi kufanya ushirikishaji zaidi na wananchi ili uweze kufanikiwa bila vikwazo. “Kuna wakati tulihisi kuwa serikali imetusahau watu wa vijijini lakini sasa tunafarijika kuona hawa REA na TANESCO wanakuja kutuunganishia umeme na tayari wameanza kuchimba mashimo kwenye kijiji chetu shughuli iliyobaki ni kufukia nguzo ,uhakiki ulishafanyika hapo awali” Alisema Parirong’o Sipitieki ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Ingoikumeni
 Afisa Uhusiano na Huduma kwa wateja ,TANESCO  Arusha,Benedict Nkini (kulia) akifafanua jambo juu ya kifaa cha kujiunganishia umeme bila kusambaza waya kinachofahamika kitaalamu kama Ready Board ,kulia ni Afisa Masoko  wa Tanesco,Adelina Lyakurwa akiwa ameshika kifaa hicho ,pia  walizungumza na wananchi wa Vijiji vya Meserani juu na chini  kuhusu  mpango wa kuwaunganisha wananchi waishio vijijini  na huduma ya umeme kwa unaotekelezwa kwa awamu ya pili katika wilaya za Arumeru,Karatu,Monduli na Longido uliofadhiliwa na REA , lengo ni kuhakikisha wananchi waishio vijijini wanafikiwa na huduma hiyo muhimu.zilizopo mkoani Arusha
Afisa Masoko  wa Tanesco,Adelina Lyakurwa akiwa ameshika kifaa cha kujiunganishia umeme bila kusambaza waya katika nyumba  kinachofahamika kitaalamu kama Ready Board ,wakati akizungumza na wananchi  wa Vijiji vya Meserani juu na chini  kuhusu  mpango wa kuwaunganisha wananchi waishio vijijini  na huduma ya umeme kwa unaotekelezwa kwa awamu ya pili katika wilaya za Arumeru,Karatu,Monduli na Longido unaofadhiliwa na REA  lengo ni kuhakikisha wananchi waishio vijijini wanafikiwa na huduma hiyo muhimu.zilizopo mkoani Arusha.Picha na Mahmoud Ahmad wa Globu ya Jamii,Arusha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...