Na Rose Masaka-MAELEZO
Viongozi wa vyama vya siasa waliopo nje ya Bunge Maalumu la Katiba wameaswa kurejea bungeni ili kufanya maridhiano ndani ya bunge hilo.
Kauli hiyo imetolewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alipokuwa akiongea na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam.
Jaji Werema amesema kuwa wajumbe walio nje ya Bunge Maalum hawana budi kurejea bungeni na kuacha kumshinikiza Rais kulivunja bunge hilo kwani hana mamlaka ya kulivunja kulingana na sheria inayoliongoza bunge hilo.
“Sheria inasema kuwa baada ya bunge hilo linaweza kuvujwa baada ya katiba kupatikana, kinyume na hapo bunge husitishwa kufikia maridhiano na kufikia mwafaka kwa kufuata misingi ya demokrasia.” alisema Jaji Werema.
Pia Jaji Werema alisema kuwa wajumbe walio nje ya bunge hilo hawana budi kurudi ili kuendelea kujadili vipengele vingine vya rasimu ili kuweza kupata katiba iliyo bora kwa nchi na watu wake.
Aidha, Jaji Werema aliviasa vyombo habari kutumia nafasi yao ya kuwa mhimili muhimu katika uongozaji wa nchi kutokuwa na upendeleo katika utoaji wa taarifa na kuacha kuongozwa na mawazo ya wachache ili kuweza kusaidia nchi kupata Katiba Mpya kwa manufaa na maendeleo ya nchi.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema akitoa ufafanuzi wa masuala Kisheria kwa waandishi wa habari kuhusu mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya wakati wa mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema akiwaonesha waandishi wa habari Rasimu ya katiba wakati akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kisheria katika mchakato wa Katiba wakati wa mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema wakati wa mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Picha na Hassan Silayo
Ukitaka utoke mvi mapema ufuatilie siasa ya nchi yetu inaumiza kichwa
ReplyDeleteThe mdudu,hao Ukawa wanasababu za msingi ndio maana hawawezi kuludi nyie simmeamua kuendelea na huo mchakato kwa wingi wenu nahuku mkiyaweka pembeni maoni ya wananchi waliowengi kulikoni nyie sasa kwanini mnataka ukawa waludi malizeni nyie kwandio kwakila kitu lakini ikija kwa wananchi watasema hatuitaki sasa tuone nani ataumbuka,watu wanapogombana kinachofuatia ni usuluhishi lakini kwajinsi mnavyotegemea wingi wenu na kukataa serikali 3 so hata hao ukawa mnaotaka waludi waludi kwajipi hasa? Wakati tayari mshakataa serikali 3?
ReplyDeleteIvi ugumu uko wapi??hawa ukawa wamesimama ktk kufuatwa kwa kile kilichopendekezwa ktk rasimu na walishasema bila ya hivyo hawarejei...nashangazwa na juhudi zinazofanywa pasipo kuangalia kipengere kilichopendekezwa na UKAWA....badala yake naona waumini wanaombwa waliombee BMK,sijui wazee wakutana na kushauri,sijui watu wenye mahitaji maalum nao wakutana....mbona ni rahisi sana....kinachotakiwa ni kuzungumza na hilo kundi la pili ambalo limeonesha ugumu wa kutofuata kilicho ktk rasimu,kama ni maombi ,ushauri wapatiwe ili wakubari kufuata rasimu maana ndio msingi/nguzo ya kikao hiko....Kama tunasifika ktk kuwasaidia majerani kwa ushauri na mawazo tunashindwaje kuwashauri hawa ambao hawataki kufuata kilichopo ktk rasimu kwa mujibu wa UKAWA????Jamani hata hili nalo tunahitaji msaada toka nje???
ReplyDeleteWajumbe mliopo endeleeni na kazi hakuna haja ya kuwabembeleza wanaojiita ukawa.Waacheni waendelee na majungu mitaani
DeleteSasa kama hakuna uhakika wa kupatikana theluthi mbili ya kura kutoka zanzibar kwanini vikao visisitishwe ili kutafuta maridhiano Kwanza,hivi kama posho zisingekuwepo sidhani kama malumbano yangekuwepo coz katiba ni tendo la maridhiano,na kwenye hili hakuna mshindi wala mshindwa ni kwa maslahi mapana ya nchi so malumbano yataisaidia nini Nchi?...
Deletehakuna mtu anayeomba kubembelezwa....ukawa washaamua kwa sababu maalum kususia mchakato wa katiba. sasa majungu yapo wapi???!#
Delete