Serikali ya China kupitia Wizara ya Nishati na Madini imetoa ufadhili wa
nafasi kumi (10) za masomo kwa watanzania katika ngazi ya shahada ya
uzamili na uzamivu katika fani ya mafuta na gesi.
Katika shahada ya uzamili wamechaguliwa watanzania 9 kati ya 46
walioomba ufadhili ambapo katika shahada ya uzamivu amechaguliwa
mtanzania mmoja kati ya wanne waliowasilisha maombi.
Msaada huu wa masomo umetolewa na Serikali ya China kwa Tanzania
kufuatia juhudi za Wizara ya Nishati na Madini kuhakikisha kuwa Serikali
inakuwa na rasilimaliwatu ya kutosha katika kusimamia Sekta za Nishati na
Madini hasa sekta ndogo ya mafuta na gesi inayokua kwa kasi hapa nchini.
Ufadhili huu ni wa pili kupitia Wizara ya Nishati na Madini ambapo wa
kwanza ulitolewa katika mwaka wa fedha 2013/14 kwa nafasi 10 katika
ngazi ya shahada ya uzamili kwenye fani za nishati na madini ikiwemo
uhandisi migodi, uhandisi wa nishati katika mafuta na gesi. Wanafunzi hao
wanatarajia kuingia mwaka wa pili wa masomo mwezi septemba, 2014.
Nafasi hizi zimepatikana kwa ushindani baada ya kutangazwa kwenye
vyombo vya habari ambapo vigezo vilivyotumika kupata ufadhili ni aina ya
kozi aliyoisoma mwombaji katika Shahada ya kwanza au Uzamili, Chuo
alichosoma shahada ya kwanza, kiwango cha ufaulu katika shahada ya
kwanza kuanzia GPA 3.0 na Uwiano wa jinsia.
Faida ambazo Tanzania itapata kutokana na ufadhili huu ni kuongeza
wataalam katika fani za sekta za nishati na madini na hasa sekta ndogo
ya mafuta na gesi, kuongeza fursa za masomo kwa watanzania hasa kwa
kuzingatia kuwa wengi hukosa elimu kutokana na kutomudu gharama, na
kuzidi kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na China.
Watanzania waliopata ufadhili wa masomo nchini China katika ngazi ya
shahada ya uzamili na uzamivu katika fani ya mafuta na gesi wakiwa
katika picha ya pamoja na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo (katikati) na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim
Maswi (wa nne kutoka kushoto mstari wa nyuma) pamoja na watendaji
wengine wa Wizara ya Nishati na Madini mara baada ya kuagwa rasmi
katika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini.Wengine katika picha
(mstari wa mbele) ni Kamishna Msadizi Nishati anayeshughulikia Umeme,
Eng.Innocent Luoga (wa kwanza kulia), Kamishna wa Madini, Eng.Paul
Masanja (wa pili kulia), Kaimu Mkurugenzi Utawala - Bi. Caroline Musika
(wa kwanza kushoto).
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi (wa tano kutoka
kushoto waliosimama), akiwatambulisha wanafunzi waliopata ufadhili wa
masomo nchini China (baadhi hawapo pichani) waliofika Makao Makuu ya
Wizara ya Nishati na Madini na kukabidhiwa nyaraka zitakazowawezesha
kujiunga na masomo nchini China.Wanaowatazama wanafunzi hao ni
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati), Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Caroline Musika (wa
kwanza kushoto, waliokaa), Mkurugenzi Msaidizi-Rasilimali Watu, Lusius
Mwenda (wa kwanza kulia),Kaimu Kamishna Msaidizi,Maendeleo ya
Nishati, Eng. Juma Mkobya (wa pili kutoka kulia), Kamishna wa Madini,
Eng. Paul Masanja (kushoto kwa Mhe.Waziri).Wengine katika picha ni
watumishi kutoka Wizara ya Nishati na Madini na waandishi wa habari.
Bi. Erasma Rutachura, ambaye amepata ufadhili wa masomo nchini
China,ngazi ya shahada ya uzamivu katika mafuta na gesi akipokea
nyaraka zitakazomwezesha kujiunga na masomo yake mwaka
huu.Anayempa nyaraka hizo ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo (wa pili kutoka kulia).Wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu,
Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi.
Mmoja kati ya wanafunzi 10 waliopata ufadhili wa masomo nchini China katika ngazi ya shahada ya uzamili, fani ya mafuta na gesi, Faustine Matiku akipokea nyaraka mbalimbali zitakazomwezesha kujiunga na Chuo Kikuu cha Hohai cha nchini humo.Wanaomtazama ni Waandishi wa Habari.
Kumekucha ndio tunakumbuka shuka! Wakimaliza masomo gesi itakuwa au imekwisha, au mabadiliko ya teknolojia yanaifanya isiwe na thamani!
ReplyDeletePresha ya nishati safi, kama ikiendelea hii gesi na mafuta itakuwa historia, na vizazi vijavyo vitatushangaa kuwa kwanini tulichelewa kufanya mabadiliko.
Hapo ndipo nchi inatakiwa kuwekeza kwenye utafiti wa nishati nyingine ambayo ni safi. Au tunasubiri vya bure kutoka mataifa ya nje?
Tufikirie nje ya boksi! Na sisi tuna uwezo, nia na sababu ya kuwa mbele wengine!