WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameutaka uongozi wa Jiji la Mbeya uongeze mapato yake ya ndani kwa kuweka mifumo ya kisasa ya ukusanyaji mapato.

Ametoa agizo hilo jana (Jumamosi, Agosti 2, 2014) wakati akizindua stendi ya kisasa ya mabasi katika eneo la Nane Nane nje kidogo ya Jiji la Mbeya.

“Nikuombe Meya Kapunga, wewe na watu wako ongezeni mapato ya ndani ya Jiji la Mbeya. Wekeni mifumo ya kisasa ya makusanyo inayotumia teknolojia ya habari na mawasiliano, acheni kutumia risiti za kuandika wa mikono,” alisema.

Akizungumzia mradi wa stendi mpya ya mabasi, Waziri Mkuu alisema ujenzi wa stendi hiyo ni miongoni mwa kazi zilizo kwenye mradi mkubwa unaohusisha uboreshaji wa huduma na miundombinu kwenye miji na majiji saba hapa nchini (Tanzania Strategic Cities Programme).

Alisema mradi huo uliibuliwa na Serikali tangu mwaka 2006 kwa kushirikiana na Benki ya Dunia. Miji na majiji mengine yanayohusika na mradi huo ni Mwanza, Arusha, Tanga, Kigoma, Mtwara na Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...