Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa albamu ya muziki wa Injili ,Waziri Mkuu mstaafu.Mh.Frederick Sumaye akionesha albamu ya mwanamuziki nyota wa muziki wa injili hapa nchini,Rose Muhando,iliyoitwa Shikilia Pindo la yesu,mara baada ya kuizindua rasmi mbele ya maelfu ya washabiki na wapenzi wa nyimbo hizo za kiroho ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar jana.
Waziri Mkuu mstaafu.Mh.Frederick Sumaye  akifungua kasha lenye CD, wakati akizundua rasmi albamu ya mwanamuziki nyota wa muziki wa injili hapa nchini,Rose Muhando,iliyoitwa Shikilia Pindo la yesu,uzinduzi huo umefanyika jana ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee na kuhudhuriwa na maelfu ya watu mbalimbali.Pichani kati ni Mkurugenzi wa Msama Promotions Ltd,Bwa.Alex Msama sambamba na Mwimbaji nyota wa Injili,Rose Muhando wakishuhudia tukio hilo.

Uzinduzi huo ulioandaliwa na kampuni ya Msama Promotions,ulionekana kufana kwa kwa kiasi kikubwa,huku waimbaji balimbali wakiwa wameshiriki onesho hilo,lililokonga washabiki na wapenzi wa muziki huo kwa kiasi kikubwa.
Waziri Mkuu mstaafu.Mh.Frederick Sumaye akisalimiana na mwanamuziki nyota wa muziki wa injili hapa nchini,Rose Muhando,iliyoitwa Shikilia Pindo la yesu,uzinduzi huo umefanyika jana ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee na kuhudhuriwa na maelfu ya watu mbalimbali.
 Mwimbaji wa nyimbo za Injili,Rose Muhanda akiwa na  skwadi lake jukwaani wakiimba mbele ya umati mkubwa wa watu (hawapo pichani),wakati wa uzinduzi wa albamu yake mpya,uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee hapo jana,ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu  Mstaafu,Mh Frederick Sumaye.
 Waziri Mkuu  Mstaafu,Mh Frederick Sumaye na wadau wengine wakishuhudia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo wakati wa uzinduzi wa albamu mpya ya Rose Muhando iliyojulikana kwa jina la Shikilia Pindo la Yesu. 
 Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria onesho hilo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Keep up,good job,its a calling,congratulations

    ReplyDelete
  2. Hongera Rose Muhando kwa kuzindua albamu mpya tunakutakia mafanikio katika kuendeleza kipaji chako cha uimbaji.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...