WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, ameusifu Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kuhakikisha wanasimamia ujenzi wa daraja la Kigamboni.

Ujenzi wa daraja hilo umekamilika kwa asilimia 60 ambapo mpaka sasa NSSF imetoa sh. bilioni 117 kati ya Bilioni 214 zitakazokamilisha ujenzi wa daraja hilo.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam, alipotembelea daraja kuona namna ujenzi unavyoendelea, Dk. Magufuli alisema kuwa ujenzi wa daraja hilo umekutana na changamoto nyingi ikiwemo kina kilichokuwa katikati ya bahari kupoteza malighafi ya ujenzi ambapo wahandisi waliamu kufanya utafiti.

Alisema kuwa juhudi za NSSF  katika kufadhili mradi huo umewezesha changamoto zilizokuwa zikiukabili maradi huo kufanyiwa kazi.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa NSSF, Ludovick Mrosso, alisema kuwa mradi huo unatarajiwa kukamilika Julai, 2015 ambapo katika daraja zitakuwa barabara sita za magari, mbili za wapita kwa miguu.
Maradi huo unajengwa kwa kushirikisha Wizara ya Ujenzi, NSSF na Tanroads. 
Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (wa pili kulia) akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni kutoka kwa Meneja wa Mradi wa ujenzi wa daraja hilo, Mhandisi Kareem Mataka, wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja hilo.
 Mh. Magufuli akifafanua akitoa maelekezo kwa Mhandisi Kareem Mataka (kulia).
Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (wa pili kulia) akikagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni linalojengwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii  (NSSF), kwa kushirikiana na Serikali. Kulia ni  Meneja Mradi ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Kareem Mataka.
 Waziri akiwa katika zira ya ukaguzi pamoja na maofisa kutoka Wizara ya Ujenzi, NSSF pamoja na waandishi wa habari.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ludovick Mrosso akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ujenz huu wa daraja ni kazi nzuri itakayonufaisha watu wanaishi Kigamboni

    ReplyDelete
  2. Big project itachange Dar skyline kabisa.

    ReplyDelete
  3. Hongera sana Magufuli na wizara nzima ya ujenzi. Hili daraja ni kiuong muhimu sana kwa maendeleo ya Kigamboni na taifa kwa ujumla.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...