WAZIRI
wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, ameusifu Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)
kwa kuhakikisha wanasimamia ujenzi wa daraja la Kigamboni.
Ujenzi
wa daraja hilo umekamilika kwa asilimia 60 ambapo mpaka sasa NSSF
imetoa sh. bilioni 117 kati ya Bilioni 214 zitakazokamilisha ujenzi wa
daraja hilo.
Akizungumza
leo jijini Dar es salaam, alipotembelea daraja kuona namna ujenzi
unavyoendelea, Dk. Magufuli alisema kuwa ujenzi wa daraja hilo umekutana
na changamoto nyingi ikiwemo kina kilichokuwa katikati ya bahari
kupoteza malighafi ya ujenzi ambapo wahandisi waliamu kufanya utafiti.
Alisema kuwa juhudi za NSSF katika kufadhili mradi huo umewezesha changamoto zilizokuwa zikiukabili maradi huo kufanyiwa kazi.
Naye
Kaimu Mkurugenzi wa NSSF, Ludovick Mrosso, alisema kuwa mradi huo
unatarajiwa kukamilika Julai, 2015 ambapo katika daraja zitakuwa
barabara sita za magari, mbili za wapita kwa miguu.
Maradi huo unajengwa kwa kushirikisha Wizara ya Ujenzi, NSSF na Tanroads.
Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (wa pili kulia) akipata
maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni kutoka kwa Meneja wa
Mradi wa ujenzi wa daraja hilo, Mhandisi Kareem Mataka, wakati alipofanya ziara
ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja hilo.
Mh. Magufuli akifafanua akitoa maelekezo kwa Mhandisi Kareem Mataka (kulia).
Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (wa pili kulia) akikagua
maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni linalojengwa na Shirika la Taifa la
Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa
kushirikiana na Serikali. Kulia ni Meneja Mradi ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Kareem Mataka.
Waziri akiwa katika zira ya ukaguzi pamoja na maofisa kutoka Wizara ya Ujenzi, NSSF pamoja na waandishi wa habari.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ludovick Mrosso akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Ujenz huu wa daraja ni kazi nzuri itakayonufaisha watu wanaishi Kigamboni
ReplyDeleteBig project itachange Dar skyline kabisa.
ReplyDeleteHongera sana Magufuli na wizara nzima ya ujenzi. Hili daraja ni kiuong muhimu sana kwa maendeleo ya Kigamboni na taifa kwa ujumla.
ReplyDelete