Kampuni ya Msama Promotions Ltd,kwa
kushirikiana na Wizara ya habari vijana,utamaduni na michezo imetangaza neema kwa wasanii kuanza zoezi la
kuwakamata watu wanaouza nakala feki za
wasanii hapa nchini.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo,Bwana Alex Msama
amesema hayo jijini dar ,kuwa zoezi hilo limekwishaanza, na mpaka sasa wamekamatwa vijana wane katika mkoa wa Dodoma
na watatu jijini Mwanza.
‘’Kuna kazi mbalimbali ambazo
zinaibiwa kila kukicha huku wamiliki wa kazi hizo wakiendelea kushuka kiuchumi na kutoona faida yoyote ya kazi hizo,huu ni wakati kwa wasanii
kuneemeka na kazi zao.Hivyo tutahakikisha
tunafika kila mahali hata sehemu zisizofikika kirahisi na yote hii ni kuonyesha
kuwa tunajali na tunathamini kazi za wasanii wetu’’,alisema Msama kwa
msisitizo.
Alisema, nakala zote zitakuwa na
stika za TRA kuhakikisha hakuna wizi
wowote unaofanyika na unaotokea katika
kazi mbalimbali za wasanii.Stika hizo zimewekwa ili kuwabaini wale wote wenye
hulka hiyo ya kuiba kazi za wasanii .Operesheni
hiyo itafanyika bila kujali
wadhifa wake ama cheo chake,akaongeza kusema kuwa zoezi hilo ni salamu kwa wale
wote wanoatumia kazi za wasanii bila kufuata utaratibu wa sheria zilizopo.
Pia amelipongeza Jeshi la Polisi nchini
kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha
katika changamoto,na pia wamekuwa wakishirikiana nao kuhakikisha zoezi hilo linakuwa endelevu na kuzunguka
kila mkoa kuhakikisha kazi za wasanii
zinaheshimiwa na zinalindwa kwa kila namna.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...