Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Pudenciana Kisaka akizungumza
Na Denis Mlowe,Iringa
JUMLA ya sh. bilioni 1.3 zimetumika katika ujenzi wa
maabara za sayansi, hosteli za wasichana na chumba cha darasa katika shule za
sekondari za Ismani, Nyang’ro na Kalenga zilizoko katika Halmashauri ya Wilaya
ya Iringa mkoani Iringa.
Akizungumza na wahabari hivi karibuni ofisini kwake
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Iringa,Pudenciana Kisaka alisema kuwa halmashauri kupitia idara ya
elimu Sekondari imekamilisha maabara tatu za masomo ya sayansi , chumba cha darasa na hostel katika shule
hizo zilizokuwa zina upungufu wa majengo hayo.
Alisema kuwa maabara moja imejengwa katika shule ya
sekondari Ismani na ujenzi wake kukamilika kwa asilimia 100 na inatumika kwa masomo ya
Bailojia na imegharimu zaidi ya shilingi milioni 89.
Kisaka alisema shule ya sekondari Kalenga imejengewa maabara
mbili ambazo zimekamilika kujengwa na zinatumika kwa masomo ya Fizikia na Kemia
na kugharimu shilingi milioni 29.
Aidha alisema halmashauri hiyo imejenga hostel ya wasichana wa
shule ya sekondari Kalenga ambao umegharimu sh. Milioni 258 mpaka kukamilika na
ujenzi wa chumba kimoja cha darasa shule ya sekondari Nyang’oro uliogharimu sh. Milioni 13.
Kisaka akizungumzia kuhusu mapokezi ya wanafunzi wa kidato
cha tano alisema idara ya elimu imepangiwa jumla ya wanafunzi 2389 wa kidato
cha tano katika shule sita hivyo idadi imeongezeka kutoka 1433 mpaka 2389 sawa
na asilimi 156 ukilinganisha na idadi ya wanafunzi waliopokelewa kwa mwaka
2013/2014 walikuwa 1433 sawa na asilimia 93.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...