Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiweka jiwe la msingi kuashiria uzinduzi rasmi wa
barabara ya Mayamaya –Mela - Bonga Km 188.15. Wengine wanaoshuhudia tukio
hilo ni Mwakilishi wa Serikali ya Japan kushoto, katikati ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John
Magufuli, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa upande wa
Tanzania Dkt. Tonia Kandiero, Mama Salama Kikwete pamoja na Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa barabara ya
Mayamaya –Mela-Bonga Km 188.15. inayojengwa kwa kiwango cha Lami. Wengine
walioshika utepe ni Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli,
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) kwa upande wa Tanzania
Dkt. Tonia Kandiero, Mama Salama Kikwete, Mbunge wa Viti maalum kutoka Chama
cha Wananchi CUF, Mbunge wa Simanjiro Cristopher Ole Sendeka, Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi na viongozi wengine wa Kitaifa.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli watano
kutoka kulia akicheza ngoma na kikundi cha ngoma za asili cha Bicha kabla ya uzinduzi
rasmi wa barabara ya Mayamaya –Mela-Bonga Km 188.15. inayojengwa kwa kiwango
cha lami.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John
Pombe Magufuli, Mama Salama Kikwete na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema
Nchimbi. Wengine katika picha ni Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge,
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe na Mwakilishi Mkazi wa
Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) kwa upande wa Tanzania Dkt. Tonia Kandiero.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katikati
akizungumza na Mzee maarufu wa Wilaya ya Kondoa Balozi mstaafu Mustapha
Nyang’anyi kabla ya uzinduzi wa Barabara ya Mayamaya –Mela-Bonga Km 188.15.
Kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge.
Katapila likisafisha sehemu ya Barabara ya Mayamaya –Mela-Bonga
Km 188.15 inayojengwa kwa kiwango cha lami.
Taswira: ‘Mkeka mpya’ Barabara ya Bicha- Kondoa mjini
inavyoonekana mara baada ya kukamilika kwake.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kushoto
akizungumza na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge pamoja na
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) kwa upande wa Tanzania Dkt.
Tonia Kandiero muda mfupi kabla ya uzinduzi wa Barabara ya Mayamaya –Mela-Bonga
Km 188.15. Picha kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Ujenzi.
Hakika inatia moyo na kufurahisha sana kuona wizara husika ikilitilia manani suala zima la ujenzi wa bara bara zetu na kuzipelekea kuwa na muonekano na kiwangu cha kisasa. Bicha - Kondoa, nimefurahi sana kuona imefikia hatuwa na kiwango hicho, nadhani mpaka kule milimani kwetu kwa 'Dinu' jamvi hilo litakuwa limeshatandikwa. Pengezi za dhati kwa serikali na wizara husika pamoja na watendaji wake kwa jumla.
ReplyDelete