Bweni la wanafunzi katika shule ya sekondari ya Kaloleni Islamic Secondary School iliyopo eneo la Kalaloleni-Pasua katika manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro linateketea kwa moto. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema moto huo umeanza majira ya saa 2 za usiku huku chanzo chake bado hakijajulikana na ripota wetu Dixon Busagaga aliye eneo la tukio anafuatilia ajali hii na atatujulisha kila kitachojiri na kupatikana.
Kikosi cha zimamoto kimefanya jitihada za kuzima moto huo licha ya kukabiliwa na changamoto ya maji.
Mungu tunusuru na hili jinamizi la ajali, poleni sana wahanga.
ReplyDeleteMungu atajalia wawe salama, ila maghorofa Kule juu kunaulazima wa kuwekwa nondo za madirishani? ikatokea ndani ya chumba mtu Hana pakutokea tujirekebishe usalama wa majengo. Hasa ma hospitali na mashule hayo.
ReplyDeleteWhat is wrong Tanzania, every day accident, what is wrong. I do not believe so. No no no, there is something under the table. God forgive us.
ReplyDelete