Wachimabji wa Kijiji cha Mandaka wilaya ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro wakifukua Kaburi la Marehemu Stephen Assey jioni hii kwa amri ya mahakama.
Na Dixon Busagaga wa Globu
ya Jamii Kanda ya Kaskazini
Uamuzi wa kufukuliwa kwa kaburi hilo umefikiwa baada ya mke anayedaiwa kuwa ni wa ndoa wa marehemu Stephen Assey, Bi. Lucy Laurant kwenda mahakamani kuweka zuio la kuzikwa kwa marehemu katika eneo ilipo nyumba aliyokuwa akiishi na mke mdogo aliyefahamika kwa jina la Fortinata Lyimo.
ya Jamii Kanda ya Kaskazini
Uamuzi wa kufukuliwa kwa kaburi hilo umefikiwa baada ya mke anayedaiwa kuwa ni wa ndoa wa marehemu Stephen Assey, Bi. Lucy Laurant kwenda mahakamani kuweka zuio la kuzikwa kwa marehemu katika eneo ilipo nyumba aliyokuwa akiishi na mke mdogo aliyefahamika kwa jina la Fortinata Lyimo.
Kutokana na hali hiyo mahakama ya Hakimu mkazi Moshi iliamuru kufukuliwa kwa kaburi na mwili kuhifadhiwa hosptali hadi pale uamuzi wa mwisho utakapofanywa na mahakama hiyo.
Globu ya Jamii kama kawaida yake itaendelea kuwapasha kila kitachojiri baada ya hatua hii ya kisheria.
Globu ya Jamii kama kawaida yake itaendelea kuwapasha kila kitachojiri baada ya hatua hii ya kisheria.
Askari Polisi wakisimamia zoezi la ufukuaji wa Kaburi hilo.
Msalaba uliokuwepo kwenye Kaburi hilo ukiwa pembeni.
Wivu ni maradhi yasiyo dawa. Haina haja ya kugombea maiti.
ReplyDeletekuna faida gani itakayopatikana hapa enyi jamani?
ReplyDeleteMbona mnakuwa ma hakimu wa kuhukumu hapa duniani?? Hizo tabu mnazoipa hiyo maiti ni kwa sababu gani???? Mwacheni akahukumiwe na Mungu kwa Matendo yake ya duniani. Bi Mkubwa, hiyo gharama unayotumia ingekusaidia kuendeleza gurudumu la maisha.
ReplyDeleteHivi ukimzika katika compaund yako, atafufuka aje akuombe msamaha au aishi na wewe maisha mengine???
Achana na hayo majanga, yaliopita yamepita ganga yajayo
Dah Dunia inaelekea wapi jamani sasa huyo marehemu wakamuhifadhi tena wakati alishazikwa? mambo gani haya.
ReplyDeleteKilicho cha muhimu siku zote ni sheria kufuata MKONDO; kama watanzania tutajitoa na kukubali kuziachia nafasi njia sahihi za kisheria basi tutafikia hatua muhimu sana. Siku zote tukumbuke kuwa tunafikia katika matatizo mengi kwa kuzuia sheria ama sera tulizojiwekea kuchukua nafasi. Kwa mantiki hiyo basi NI SAHIHI kufukua kaburi na KAMA JAJI ama HAKIMU ATARIDHIA KISHERIA basi MAREHEMU ATAFUKIWA TENA. Watanzania wenzangu umuhimu wa kusimamia haki, unatimia pale tu sheria zinapofuatwa pamoja na kuwa kufuata sheria KUNA GHARAMA kuu kama hizi za kufukua makaburi. Ukweli utabaki pale pale ni muhimu kwa HAKI KUTENDEKA, na ili haki itendeke SHERIA zinatumika kusimamia na matokeo yake ndio kama haya.
ReplyDelete