AISHA Fathi ‘Aisha Bui’ anafunguka kwa kutamba kuwa filamu yake mpya inayoingia sokoni leo, itadhihirisha kipaji chake katika tasnia ya filamu, kwani amewakilisha wazo lake moja kwa moja bila kupigwa alichoandika. Ingekuwa ni kazi ya kushirikishwa isingekuwa rahisi.
“Najua kila mtu anakuwa na uwezo wake katika filamu lakini unaweza kushindwa kufanya hivyo kwa sababu ya kukosa nafasi ndio maana mimi nimeamua kutumia kampuni yangu kutimiza ndoto zangu. Wiki hii Yuneda Entertainment wanasambaza kazi yangu mtaani,”anasema Aisha Bui.
Sinema hiyo ya Mshale wa Kifo inasambazwa na kampuni ya kizalendo ya Yuneda Entertainment ya Jijini Dar es Salaam, ikiwa imetayarishwa na Aisha Bui chini ya kampuni yake ya Badgirl Entertainment, na hii ni filamu yake ya kwanza mwanadada huyu.
Filamu ya Mshale wa Kifo inawakutanisha wasanii nyota wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu Bongo kama vile Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’, Mzee Korongo, Salim Ahmed ‘Gabo’, Aisha Bui na wasanii wengeine wakali. Aisha anasema pia anazindua kampuni yake ya Badgirl Entertainment inayotoa filamu ya Mshale wa Kifo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...