Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) Prof. Emanuel Mjema akizungumza wakati wa hafla ya kuwakaribisha waliokuwa wanafunzi wa chuo hicho waliohitimu miaka iliyopita wakati wa mwendelezo wa shughuli mbalimbali za chuo hicho kutimiza miaka 50.
Bw. Alexander Msofe akizungumza na wahitimu wa miaka ya nyuma wa chuo cha CBE kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi wakati wa hafla ya kuchangia maendeleo ya CBE iliyowahusisha wahitimu hao jijini Dar es salaam.
Bw. Isdori Kwayi, mmoja wa wahitimu wa chuo cha CBE mwaka 1972 akitoa mchango wake kuhusu namna chuo hicho kinavyoweza kukusanya fedha kutoka katika vyanzo mbalimbali ili kuboresha miundombinu yake wakati wa hafla fupi iliyowahusisha wahitimu wa chuo hicho jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wahitimu wa CBE wa miaka iliyopita wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa hafla ya kuchangia maendeleo ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam ambacho kimetimiza miaka 50.
Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...