Na: Geofrey Tengeneza

Taasisi na makampuni kadhaa yameendelea kujitokea kudhamini onesho la kimataifa la utalii la Swahili ‘Swahili International Tourism Expo’ (SITE) linaloandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na ambalo linatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City kuanzia Oktoba 1 – 4, 2014.

Aidha Bodi ya Utalii Tanzania imesema milango bado ipo wazi kwa makampuni na taasisi mbalimbali za serikali na binafsi kuwaunga mkono kwa kujitokeza kudhamini onesho hili linalofanyika kwa mara ya kwanza.

Licha ya wadhamini wakuu wa onesho hilo ambao wako kiwango cha platinum shirika la hifadhi ya taifa (TANAPA), mamlaka ya hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) pamoja na shirika la ndege la Ethiopia, wadhamini wengine katika viwango vya dhahabu (Gold) na Silva (sliver) ni pamoja Zanzibar collection, Hoteli za Sea Cliff, Serena hotel, Southern Sun, New Africa, Hyatt Regency, Protea, Serena Bouganvillea Safari lodge, Acacia Farm lodge na Soroi Tented Camp zimedhamini huduma ya malazi kwa wageni maalumu ambao ni wafanya biashara wakubwa wa kusafirisha watalii kutoka Marekani, Uingereza, Ujerumani n.k pamoja na wandishi wa habari wa kimataifa wanaokuja kwa ajili ya onesho hilo.

Wakati Wizara ya mambo ya nje na Uhusiano wa kimataifa ikitoa udhamini wa mabasi ya kubebea washiriki wakati wa onesho hilo, benki ya CRDB imetoa udhamini wa fedha taslimu na inatarajiwa kuwa na banda ndani ya maonesho hayo ya aina yake.

Kwa upande wa usafiri wa ardhini utadhaminiwa na makapuni Zara Tours, Naeda Safaris Ltd, Wildlife Expedition Safari, huku Azam Marine wakijitokeza kudhamini usafiri wa baharini kutoka Zanzibar. Mashirika ya ndege ya Rwandair, Precision Air na Uturuki (Turkish airline) yatatoa tiketi za ndege kwa ajili ya kuwasafirisha baadhi ya wageni wakati wa onesho hilo.

Makampuni mengine yaliyojitokeza ni yale yanayomiliki majarida. Haya ni Event, Dar Life na 7th Kenya,ambavyo vinatangaza onesho hili kupitia majarida yao. Aidha kampuni ya Montage imetoa udhamini wa kuwa mpambaji katika kumbi za mikutano. Boogie woogie pia wametoa udhamini na watakuwa na mgahawa wao wa chakula katika banda la utalii wa utamaduni ilhali wadhamini wengine Black Tomato wao watakuwa na banda la kuuza kahawa ya Tanzania.

‘Swahili International Tourism Expo’ litakuwa likifanyika kila mwaka mnamo mwezi wa Oktoba na kuhudhuriwa na washiriki kutoka ndani na nje ya Tanzania. Floor Media kutoka hapa nchini na Go Places kutoka

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...