![]() |
Sensei Magoma Nyamuko Sarya |
Sensei Magoma, kama anavyojulikana na wanafunzi wake lukuki ndani na nje ya nchi ndiye aliyekuwa gwiji wa Karate na kiungo muhimu
kwa sensei Nantambo Camara Bomani (RIP) katika kuendeleza mwenendo wa Sanaa ya Karate nchini
Tanzania. Sensei Magoma (Daudi) amefundisha wanafunzi wengi wa Karate wa kiTanzania zaidi ya mwalimu yeyote mwingine hapa nchini.
Amekuwa mwanafunzi kiongozi mwenye
mamlaka kamili ya kusimamia Dojo lililopo katika shukle ya Msingi ya Zanaki (awali dojo hilo lilikuwa katika shule ya Sekondari ya wasichana ya Zanaki jijini Dar es salaam na matawi yake yote ya Tanzania tokea mwaka 1976 hadi
1982.
Sensei Magoma ni mmoja kati ya wanafunzi wa tano wa kwanza nchini Tanzania kupata shahada ya
kwanza (“Shodan”) mkanda mweusi mwaka 1976 akiwa mwenye umri mdogo kuliko wenzake wote chini ya sensei Bomani. Wanafunzi hao ni: Sensei Mapfumo Gamanya
( Mzibabwe), sensei Tola Sodoinde Malunga, Sensei Abome Mabruki na kaka yake
sensei Adombe Mabruki.
.jpg)
Wakati sensei Bomani akiwa huko nchini Marekani kuanzia mwaka 1976
hadi mwaka 1981 sensei Magoma ndiye alikuwa mwanafunzi mkuu kiongozi na
mwenye mamlaka yote ya mapendekezo na kutoa test na hata mikanda yote ya mtindo
wa Okinawa Goju Ryu Kyokai chini ya mfumo wa kiongozi wao wa Karate duniani
Master Eiichi Miyazato, mwalimu wa sensei Bomani.
Ni vigumu mno kuwataja wanafunzi wote waliopitia chini yake, bali tu, kila mwanafunzi aliyekuwa dojo kwa miaka ya 1976 hadi 1982 alikuwa chini ya himaya yake. Hao ni pamoja na Sensei Rumadha Fundi anayefanya vyema sana huko Marekani, hali kadhalika Edgar Kaliboti ambaye anang'aa nchini Australia.
Ankal pia alikuwa mmoja wa wanafunzi wa Sensei Magoma kwa miaka kadhaa, na hadi sasa anajivunia uanafunzi wake ambapo haukuwa wa kurusha ngumi na mareke tu, bali pia aliwajenga wanafunzi kifikra na kimwili kwa kuwafunza mazoezi ya hali ya juu ya Yoga.

Licha ya kuwa mkufunzi mkuu wa Karate nchini Tanzania, mara tu baada ya kuondoka kwake mwaka 1982 hapa nchini kuelekea nchi za mashariki ya mbali ikiwemo, India,
Nepal, Singapore, Malaysia na Phillipines. Mwalimu Magoma aliacha pengo kubwa sana katika kuimarisha Sanaa ya
Karate mtindo wa Goju Ryu nchini Tanzania. Ishukuriwe kwamba wanafunzi wake kadhaa pamoja na wengine waliofuata nyuma yake wanaendeleza sanaa hiyo ya kujilinda kila siku katika dojo la Zanaki, chini ya Sensei Malekia, Sensei Geoffrey Shoo, Sensei Murudker wakisaidiwa na Sensei Almasi na wengineo.
Sensei Magoma pia ni mkufunzi wa Sanaa ya Yoga na mwenye uzoefu mkubwa katika fani
hiyo ambayo ilimpeleka nchi nyingi akiwa kama mwalimu na wakati huohuo akifundisha
Karate. Alipata mafunzo ya Sanaa ya Yoga nchini India kutoka katika chuo cha “Neo-
Humanist Studies” katika mji wa Varanasi, mwaka 1983.
Mengi aliyoyafanya akiwa bado yupo nchini kwa wakati huo, ni pamoja na kutenganisha darasa
la mafunzo ya Karate la watoto na watu wazima na kuliita kwa jina ka heshima ya
mwanzilishi wa shule hiyo “ Bomani Brigade” au “BB” kama ilivyokuwa anaitwa.
.jpg)
Sensei Magoma, ni mwalimu mwenye upeo wa hali ya juu sana katika Sanaa ya Karate
ya Okinawa Goju Ryu Karate-do Jundokan Kyokai na kama nilivyoeleza hapo awali,
ameacha pengo kubwa mno ambalo sasa ni dhahiri kwamba kurejea kwake katika
kufundisha sanaa hii nchini, kunaweza kuwahamasisha walimu wengi na kuiga mfano
wake wa kuwa na moyo na nia ya kusaidia vijana na kuwapa nishani katika maisha yao
ya baadae.
Kwa mengine Zaidi yanayohusika na Sensei Magoma na jinsi yakuwasiliana nae yatafuatia hao baadae.
Sensei Magoma (fulana ya rangi ya chungwa) akiwa mgeni rasmi katika sherehe za kuadhimisha miaka 37 ya Dojo la Zanako Aprili 20, 2010. Kulia kwake ni Sensei Heri Kivuli
Sensei Magoma (fulana ya rangi ya chungwa) akilishwea keki na mmoja wa wanafunzi wake Ambaye ni Ankal katika sherehe za kuadhimisha miaka 37 ya Dojo la Zanako Aprili 20, 2010. Kulia kwake ni Sensei Heri Kivuli

Kiongozi mkuu wa Dojo hilo hivi sasa Sensei Malekia akiwa na Japhet Kaseba ambaye pia ni mwanafunzi mwandamizi katika shule hiyo.
Na kupata habari za nyuma kuhusu Goju Ryu Karate nchini Tanzania
uncle kumbe na wewe upo fiti. nitakuja kujaribu siku moja km vile putin alipoenda japan akzipiga kidogo.,,,
ReplyDelete