Jaji Constancia Gabusa (wa sita kutoka kushoto) akizungumza na mtoto Abdalah Suleman (kulia) aliyefika kisimani kuchota maji katika kijiji cha Chanjagaa wilayani Same. Mradi wa kisima hicho unafadhiliwa na kampuni ya uchimbaji wa madini aina ya bauxite ya Willy Enterprises Ltd.
Muuguzi wa zahanati ya Mteke iliyopo wilayani Same Bi. Winfrida Momoya (kulia) akizungumza na majaji Bw. Venance Bahati ( wa pili kutoka kushoto) na Bi Constancia Gabusa (wa tatu kutoka kushoto) mara walipotembelea zahanati hiyo inayofadhiliwa na kampuni ya uchimbaji wa madini aina ya bauxite ya Willy Enterprises Ltd.
Mkurugenzi wa mgodi wa madini ya vito wa TanzaniteOne Bw. Farai Manyemba akielezea mchango wa kampuni hiyo katika huduma za jamii mara timu ya majaji na sekretarieti ilipofanya ziara kwenye mgodi huo.
Timu ya majaji na sekretarieti ikiangalia bidhaa za urembo zinazotengenezwa na kikundi cha wakinamama wa kimasai cha Ebeneza mara walipotembelea kikundi hicho huko Mirerani. Kikundi hicho kinafadhiliwa na kampuni ya TanzaniteOne ikiwa ni pamoja na kutangaza bidhaa zake nchini Marekani.
Jaji Constancia Gabusa (kushoto) akioneshwa urembo na kupewa maelezo na mama wa kimasai ambaye jina lake halikupatikana mara moja juu ya shughuli zinazofanywa na kikundi cha wakinamama wa kimasai cha Ebeneza kinachofadhiliwa na kampuni ya TanzaniteOne.
Mkazi wa kijiji cha Kolila, King’ori Bw. Petro Losina akitoa maelezo kuhusu kisima cha maji kilichofadhiliwa na kampuni ya usagaji wa kokoto na utengenezaji wa matofali ya Arusha Aggregates Ltd. mbele ya majaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...