Gari aina ya Landusider lenye nambari za usajili T540 APN lililokuwa likitokea Temeke kuelekea Tazara, Dar es salaam lilipinduka jana wakati dereva wa gari hilo alipokuwa akijaribu kulikwepa Lori lililokuwa limeegeshwa pembeni ya barabara wakati akiwa kwenye mwendo kasi.Dereva huyo alikuwa akilikimbiza gari lingine aina ya Canter moja (namba zake za usajili hazikufahamika mara moja) lililokuwa likitokea Temeke nalo likiwa na mwendo kasi, na hata baada ya gari lake kupinduka dereva huyo alitoka upesi upesi bila kuijali afya yake na kisha kuchukua bodaboda na kuendelea kuifukuza ile Canter. Picha na Evance Ng'ingo wa Habari5blog
Askari Polisi akijaribu kufanya mawasiliano na wenzake wakati wa ajali hiyo,huku mashuhuda wakiwa wamelizunguka gari hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...