Mkurugenzi Mtendaji wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu Gold Mine Bw. Peter Burger ( wa kwanza kushoto) akizungumza na jopo la majajaji na sekretarieti iliyotembelea mgodi huo kwa ajili ya kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Ibanza Bw. Dions Kagiye (katikati) akizungumza na baadhi ya majaji waliotembelea shule hiyo inayofadhiliwa na mgodi wa Bulyanhulu Gold Mine kwa ajili ya kuifanyia tathmini.
Mmoja wa majaji Dkt. Yohana Mtoni (kushoto) akimsaidia mmoja wa watoto waliofika katika kisima cha maji cha Ilogi kuvuta maji. Kisima hicho kinafadhiliwa na mgodi wa Bulyanhulu.
Meneja Mahusiano wa Mgodi wa Buzwagi uliopo Kahama, Shinyanga Bi. Dorothy Bikurakule ( wa kwanza kulia mbele) akiongoza jopo la majaji na sekretarieti kutembelea kituo cha afya cha Mwendakulima kinachofadhiliwa na mgodi huo.
Meneja Mahusiano wa Mgodi wa Buzwagi uliopo Kahama, Shinyanga Bi. Dorothy Bikurakule (katikati) akielezea mchango wa mgodi huo katika uwezeshaji wa kikundi cha vijana cha ufyatuaji wa matofali cha Mwendakulima.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mwendakulima Bi. Diana Kuboja akielezea mchango wa mgodi wa Buzwagi Gold Mine katika ujenzi wa shule hiyo kwa majaji na sekretarieti iliyotembelea shule hiyo kwa ajili ya kufanya tathmini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. DADA KWELI WEWE NI MTU WA KAZI MAVAZI YAKO YAKO KIKAZI,KWELI WEWE JEMBE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...