Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, SACP AHMED Z. MSANGI (pichani) anawatangazia Wananchi wote ya kuwa vijana waliomaliza Kidato cha Nne mwaka 2013 na cha Sita mwaka 2014 na kuchaguliwa kufanya usalii wa kujiunga na Jeshi la Polisi, Usaili huo utafanyika kuanzia Tarehe 28.09.2014 hadi Tarehe 01.10.2014 kuanzia majira ya saa 08:00 Asubuhi hadi saa 16:00 jioni katika Shule ya Sekondari Mbeya Day.

Muhimu:
·         Mwombaji aliyeitwa kwenye usaili aje na vyeti vyake vyote vya masomo [(Academic Certificate(s)/Results slip(s) & Leaving certificate(s)], nakala halisi ya cheti cha kuzaliwa (Original Birth certificate). Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.
·         Mwombaji awe na namba ya simu itakayotumika kumjulisha endapo atachaguliwa.
·         Kila mwombaji aliyeitwa kwenye usaili atajigharamia usafiri, chakula na malazi kwa muda wote wa zoezi la usaili. Pia waombaji waje na kalamu za wino kwa ajili ya usaili wa kuandika.
 Ni muhimu sana kwa kila mwombaji kuzingatia tarehe ya usaili na muda wa kuanza usaili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...