1. UTANGULIZI
Binadamu hakuumbwa katika ombwe, ameumbwa akiwa katika dimbwi la majukumu, kwake binafsi, familia, jamii na dunia kwa ujumla. Wachache sana wanaoweza kupitia ngazi zote za uwajibikaji huu. Katika hao wachache, hatutasita kumtaja Jakaya Khalifan Mrisho Kikwete. Ili kujijenga vema katika misingi ya uongozi, Jakaya Kikwete alijijenga vema katika taasisi hizi za msingi na alipikwa vema.
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ni aina ya kiongozi pekee ambaye alihudumu nafasi mbalimbali ndani ya chama na serikali. Safari yake ya uongozi ilianzia ndani ya chama cha TANU. Alikuwa kiongozi wa Vijana wakati wa TANU na baadaye CCM hadi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi. Wakati wote katika nafasi zake kwenye chama na serikali, Mh. Kikwete alihimiza maendeleo katika Jimbo lake na watanzania kwa ujumla.
Kimsingi amekuwa chachu ya maendeleo katika kipindi cha urais wake kuanzia mwaka 2005 hadi 2014 ambapo ameshatekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo ambapo mingi imeshakamilika na mingine inategemewa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2015.
Huyo mama amekubaliana na wazungu wanaosema let us give credit were it is due. Kwa kiswahili...Kiongozi akiongoza tukapiga hatua na kutuunganisha ni vizuri kutochukulia tu hivi hivi.
ReplyDeleteHuyu dada nguo yake nzuri, amependeza kweli.
ReplyDeleteKwa kweli hamna maendeleo ya maana kwani sasa wameongeza div 5 yani kufeli kumezidi hivyo kizazi kkijaco kina kazi kweli. Maendeleo yangetokea kama serikali ingepunguza wabunge na vyeo vusivyokuwa na maana....
ReplyDelete