Kwa namna ya pekee tunakukumbuka mtoto wetu FLORA FLOWIN
MKANULA kwa kuitwa na Mwenyezi Mungu tarehe 10 Septemba, 2013.
Ni mwaka mmoja sasa tangu ututoke. Upendo wako, ucheshi wako,
ushauri wako, uvumilivu wako utakumbukwa daima na sisi wazazi wako
Baba FLOWIN na Mama ALICE.
Unakumbukwa pia na wadogo zako, IRENE na CARRINE, Marafiki,
Wanafunzi wenzio wa ‘PCB’ pamoja na familia ya ST. JOSEPH
CATHEDRAL HIGH SCHOOL. Kwa hiyo siku ya Jumatano tarehe 10
Septemba, 2014 itaazimishwa Misa Takatifu Kinondoni Makaburini
tukiwa na familia ya ST. JOSEPH CATHEDRAL HIGH SCHOOL
saa 3.00 asubuhi, na baadae tutaenzi siku yake kwa maadhimisho
yatakayofanyika mchana saa 7.30 ST. JOSEPH CATHERDRAL HIGH
SCHOOL kwa nia ya kumshukuru Mungu kwa zawadi ya FLORA
FLOWIN MKANULA.
“Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lipewe sifa”.
“AMINA”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...