Kituo cha redio kinachokuja juu kwa kasi nchini Tanzania cha EFM 93.7 kimeendelea na road show yake kabambe inayokwenda kwa jina la MUZIKI MUNENE ambapo kila Jumamosi kinachagua kiota kimoja cha maraha sehemu mbalimbali nchini na kwenda kuwaburudisha wasikilizaji wake wanaoongezeka siku hadi siku. 
Libeneke hilo lilianzia Bagamoyo Jumamosi ya wiki iliyopita, na Jumamosi ya wiki hii walikuwa Kibaha Container, huko huko mkoa wa Pwani. Msemaji wake Dennis Ssebo anasema mambo ni mswano sana kwenye road show hiyo ya aina yake inayoambatana na muziki mnene na vyombo na jukwaa la kisasa kabisa. 
Anasema Jumamosi hii inayokuja libeneke la  MUZIKI MUNENE litahamia Ukonga Recreation Centre jijini Dar es salaam. Pamoja na Ma-DJ wake wa nguvu kiburudisho kingine ni MKUDE SIMBA na vibweka vyake...

  Kibaha Container kulikucha Jumamosi iliyopita 
Wasikilizaji wa EFM 93.3 wa Ukonga wanaambiwa wakae mkao wa kula Muziki Munene waja Jumamosi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...