Mama Dora Msechu Mheshimiwa Balozi wa Tanzania nchi za Nordic na Baltic alipokelewa kwa shangwe mwihoni mwa juma ambapo  Watanzania kibao walifika kutoka karibia kila kona ya Sweden. 
Siku ilianza kwanza na mkutano na Mama Dora Msechu kujitambulisha rasmi kwawatanzania. Baada ya mkutano kulikua na chakula na Dansi kusherekea Tanzania day. Kivutio kingine kikubwa ni umahiri wa maDJ wakali hapa Sweden wakitambulika kwa majina ya Dj Richie na Dr Erick Kalebi ambao walitumbuiza mziki wa wasanii mbalimbali kutoka Tanzania bila kusahau Aina mbalimbali za miondoko kama vile Mduara , sebene na mengineyo mingi. 
Sherehe ilianza saa kumi kwa wageni kuingia ukumbini. na nusu saa baadaye Mh Balozi aliingia ukumbini na wimbo wa Taifa ukapigwa .Watu walisimama kumkaribisha. 
Baada ya hapo  Mc alianza kutoa utangulizi wa mkutano pamoja na ratiba. Baada ya hapo ilifuatia wakati wa Mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania Sweden Mh Tengo Kilumanga kumkaribisha rasmi Mh Balozi.
Ikafuata hotuba nzuri ya Mh Balozi ambayo ilifuatiwa na risala ya Jumuiya ya WaTanzania pamoja na hotuba ya Mwenyekiti wa chama cha wanafunzi Sweden. Baada ya hapo yalifuata maelezo ya historia ya chama yaliyotolewa na dada Seynab. Kulikuwa na uhamasishaji kuhusu umuhimu wa kujiunga na Jumuiya . Baada ya hapo Mh Balozi alifunguwa mziki,vinywaji na chakula. Mnuso ukanoga.
Balozi wa Tanzania nchi za Nordic na Baltic Mhe Dorah Msechu (katikati) akiwa na baadhi ya wanajumuiya ya Watanzania nchini Sweden wakati wa sherehe hizo
Balozi wa Tanzania nchi za Nordic na Baltic Mhe Dorah Msechu akijumuika na wanajumuiya kulisakata rhumba
Kila mmoja alikuwa na furaha kwa siku hii adhimu. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hivi wabongo bado wako bongo? Naona tuko kila mahali, si PNG, Ukraine etc etc

    ReplyDelete
  2. Poa sanaaaa

    ReplyDelete
  3. Watanzania wanasoma na kufanya kazi katika nchi nyingi tu. Hata usafiri visiwa vya Pacific au Carribean utawakuta.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...