Na Veronica Simba – Dar es Salaam
Maafisa Wakuu 35 kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa cha Afrika Kusini
(South African National Defence College – NDC), wametembelea Makao
Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini Septemba 30, 2014 kwa lengo
la kujifunza kuhusu Sera ya Tanzania kuhusu vyanzo vya nishati nchini
hususan mafuta, gesi, makaa ya mawe na uvumbuzi wa madini mengine
na changamoto zake.
Maafisa hao waliongozwa na Mkuu wa Chuo Brigedia Jenerali G.M. Yekelo
pamoja na Maafisa kutoka jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
ambao ndiyo wenyeji wa wageni hao hapa nchini.
Wakiwa Wizarani, Maafisa hao walipokelewa na Viongozi na Maafisa
Waandamizi wa Idara za Nishati na Madini na kupewa maelezo mafupi
kuhusu vyanzo vya nishati nchini pamoja na rasilimali za madini.
Ujumbe huo upo nchini kuanzia Septemba 27 kwa ziara ya mafunzo na
wanatarajia kurejea Afrika Kusini Oktoba 2, 2014.
Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa cha Afrika Kusini (South African
National Defense College – NDC), Brigedia Jenerali G.M. Yekelo akiuliza
swali kuhusu rasilimali ya gesi asili kwa Kamishna Msaidizi wa Gesi,
Mhandisi Nobert Kahyoza (wa kwanza kushoto).
Mmoja wa Maafisa kutoka Chuo cha NDC akitoa salamu za shukrani kwa
Wizara ya Nishati na Madini kwa niaba ya wenzake.
Kamishna Msaidizi wa Gesi, Mhandisi Nobert Kahyoza (kushoto), akipeana
mkono na mmoja wa Maafisa kutoka NDC, baada ya kukabidhiwa zawadi
kwa niaba ya Wizara ya Nishati na Madini.
Kamishna Msaidizi wa Gesi, Mhandisi Nobert Kahyoza akitoa maelezo
kuhusu Kitabu chenye kueleza rasilimali za madini yaliyopo Tanzania kabla
ya kukikabidhi kama zawadi kwa Ujumbe wa Maafisa wa NDC.
Kamishna Msaidizi wa Gesi, Mhandisi Nobert Kahyoza akitoa neno la
shukrani kwa niaba ya Wizara ya Nishati na Madini kwa Ujumbe wa
Maafisa kutoka NDC waliofika kutembelea Wizarani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...